Thursday, November 23

Museveni awapandisha vyeo maofisa 300 wa jeshi


Kampala, Uganda. Rais Yoweri Museveni wa Uganda amewapandisha vyeo maofisa 300 wa jeshi, akiwamo Mkuu wa Usalama Jeshini (CMI), Kanali Abel Kandiho aliyepandishwa kuwa Brigedia.
Pia, yumo Kamanda wa Kikosi Maalumu, Kanali Don Nabasa ambaye sasa anakuwa Brigedia.
Brigedia John Mateeka amepandishwa cheo kuwa Meja Jenerali akiwa miongoni mwa majenerali wapya watano waliopandishwa vyeo.
Wakati huohuo, polisi nchini Uganda wamelifunga gazeti la habari za udaku la The Red Pepper na kuwatia mbaroni baadhi ya wafanyikazi wake.
Wakurugenzi wakuu watano wa gazeti hilo wanashikiliwa na polisi pamoja na wahariri kadhaa.
Kukamatwa kwao kunatokana na taarifa iliyochapishwa na gazeti hilo inayodai Rais Museveni alikuwa akipanga njama za kupindua utawala wa Rwanda.
Madai hayo yamekanushwa na Serikali ya Uganda.

No comments:

Post a Comment