Wednesday, November 15

Mugabe azuiliwa na wanajeshi nyumbani kwake na wanajeshi Zimbabwe

Young women walk past an armoured personnel carrier in Harare, 15 NovemberHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWanajeshi wanashika doria barabara za mji mkuu Harare
Jeshi nchini Zimbabwe linamzuilia Rais Robert Mugabe kwake nyumbani katika mji mkuu wa nchi hiyo Harare, Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma amesema.
Bw Mugabe alimwambia bw Zuma kwa njia ya simu kwamba yuko salama, kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa afisi ya Zuma.
Wanajeshi wanashika doria katika barabara za Harare baada ya kuchukua udhibiti wa runinga ya taifa katika kile walichosema ni juhudi za kuwaandama "wahalifu".
Hatua hiyo huenda ikawa juhudi za kutaka kumuondoa madarakani Bw Mugabe na badala yake kumuingiza madarakani makamu wake wa rais Emmerson Mnangagwa, ambaye alimfuta kazi wiki iliyopita, waandishi wa BBC wanasema.
Kufutwa kwa Bw Mnangagwa wiki iliyopita kulikuwa kumemuweka mke wa Rais Mugabe, Grace, katika nafasi nzuri ya kumrithi.
Bw Mugabe, 93, ameongoza taifa hilo tangu lilipojipatia uhuru mwaka 1980 kutoka kwa Uingereza.
Wanajeshi nchini Zimbabwe walichukua udhibiti wa kituo cha taifa cha utangazaji usiku na milipuko mikubwa ilisikika pamoja na ufyatuaji wa risasi usiku kucha mjini Harare.
Jenerali mmoja wa jeshi alitokea kwenye runinga na kusisitiza kwamba hakujatekelezwa mapinduzi ya kijeshi.
Alisema Rais Robert Mugabe na familia yake "wako salama salimini."
Harare
Nini kimetokea?
Kuna taarifa kwamba wanajeshi wanatumia vifaru na magari ya kivita kufunga barabara karibu na majengo ya bunge mjini Harare na pia nje ya makao makuu ya chama tawala cha Zanu-PF.
Awali, milipuko pamoja na milio ya risasi vilisikika kaskazini mwa mji huo mkuu. Milio ya risasi ilisikika pia karibu na makao ya kibinafsi ya Rais Mugabe, 93.
Wanajeshi wanadaiwa kuingia katika makao makuu ya runinga ya taifa ZBC, na Meja Jenerali Sibusiso Moyo alisoma taarifa kwenye runinga ya taifa.
Alilihakikisha taifa kwamba Bw Mugabe na familia yake wako salama na kusisitiza kwamba usalama wao umehakikishwa.
Jeshi lilisema linawaandamana tu wale aliosema ni "wahalifu" wanaomzingira rais.
Alikanusha kwamba kumekuwepo na mapinduzi ya kijeshi.
Wanajeshi wakiwa na magari ya kivita viungani mwa Harare, Zimbabwe jana Novemba 14,2017Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWanajeshi wakiwa na magari ya kivita viungani mwa Harare, Zimbabwe Jumanne
Jumatano asubuhi, akaunti ya Twitter ambao inajidai kuwa ya Zanu-PF ilisema kulikuwa kumetokea "ubadilishanaji wa mamlaka bila umwagikaji wa damu".
Zimbabwe Army Gen Constantino Chiwenga, commander of the Zimbabwe Defence Forces (R), and Valerio Sibanda, commander of the Zimbabwe National Army address a media conference held at Zimbabwean army headquarters in Harare on MondayHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMaafisa wakuu katika jeshi wamekuwa wakilalamika kuhusu yaliyokuwa yakijiri nchini humo karibuni
Muda mfupi awali, akaunti hiyo ilikuwa imesema "familia ya rais" ilikuwa inazuiliwa, lakini tuhuma hizi hazikuthibitishwa.
Jumanne, maafisa wa Zanu-PF walimtuhumu mkuu wa majeshi Jen Constantino Chiwenga kwa "vitendo vya uhaini" kwa kukosoa hatua ya Rais Mugabe ya kumfuta kazi makamu wa rais Emmerson Mnangagwa wiki iliyopita.
Zanu-PF alisema msimamo wa Jen Chiwenga ulikuwa "na nia wazi ya kuvuruga amani ya taifa ... na unaashiria vitendo vya uhaini kwa upande wake na tamko lake lilikuwa na nia ya kuchochea maasi".
Jumatatu, Jenerali Chiwenga alitishia kwamba operesheni ya kuwaondoa wanaompinga rais katika chama tawala inafaa kusitishwa la sivyo jeshi lingeingilia kati.
Nini hakijatokea?
Hakujakuwa na tamko lolote kutoka kwa serikali kuhusu yanayojiri - jambo ambalo linaashiria kwamba huenda ni kweli Mugabe na watu wake hawana udhibiti tena wa serikali, wachanganuzi wanasema.
Na kwa sasa hakuna taarifa zozote kwamba kikosi cha Walinzi wa Rais, ambacho humtii Bw Mugabe, kimeingilia kati.
Iwapo walinzi wake wangeingilia kati, bila shaka kungekuwa na umwagikaji wa damu.
Haya ni mapinduzi ya kijeshi?
Ni hatua ambayo imetajwa kama "ya kubahatisha sana" na mwandishi wa BBC anayeangazia kusini mwa Afrika Andrew Harding.
Anasema ni muhimu kukumbuka kwamba Bw Mugabe sasa hatishiwi na nchi za magharibi ambazo amekuwa akiwaonya raia wake dhidi yake kwa miongo mingi, au na wanasiasa wa upinzani nchini Zimbabwe au hata na maasi ya raia kutokana na hali ngumu ya kiuchumi.
Robert Mugabe (R) na Grace Mugabe 9 Novemba 2017Haki miliki ya pichaAFP
Image captionMajaribio ya Bw Mugabe kumuweka mkewe katika nafasi ya kumrithi imewakera wengi katika Zanu-PF na katika jeshi
Na kwa mujibu wa Harding, mzozo wa sasa umetokana na mvutano wa ndani ya chama cha Zanu-PF. Atakayeibuka na ushindi anaweza kutarajia kwamba chama, baada ya kutakaswa, kitamfuata.
Kwenye hotuba yake kupitia runinga, Meja Jen Moyo alisema angependa ieleweke wazi kwamba "jeshi halijatwaa udhibtii wa serikali, Tunajaribu kutatua mzozo wa kisiasa, kijamii na kiuchumi katika taifa letu."
Amesema nchi hiyo itarejea katika hali ya kawaida hivi karibuni baada ya jeshi kutimiza alichosema ni "lengo" lake.
Nini kimechangia hatua ya sasa?
Robert Mugabe na Emmerson Mnangagwa during celebrations marking his birthday at the Great Zimbabwe monument in Masvingo on 27 February 2016Haki miliki ya pichaAFP
Image captionMakamu wa rais Mnangagwa na Robert Mugabe walipokuwa bado marafiki Februari 2016
Bw Mugabe anapoendelea kuzeeka na kupoteza udhibiti wa nchi yake, macho yote yamekuwa yakiangazia nani atamrithi.
Inaonekana kana kwamba hatua ya jeshi imechochewa na kufutwa kwa makamu wa rais Emmerson Mnangagwa wiki iliyopita.
Amekuwa ndiye mpinzani mkuu kwa Grace Mugabe, mume wa Rais Mugabe ambaye ni mdogo wake kwa miaka arobaini.
Bw Mnangagwa ni wa kizazi cha wazee ambao waliongozwa vita vya ukombozi nchini Zimbabwe miaka ya 1970 na kuchangia uhuru wa Zimbabwe kutoka kwa Uingereza mwaka 1980 ambapo Mugabe aliongoza akiwa waziri mkuu na baadaye kama rais.
Maj Gen Sibusiso Moyo speaking on ZBC, 15 November 2017
Image captionMeja Jenerali Sibusiso Moyo
Kundi hilo la wazee linapingwa na kizazi cha vijana wanaojiita "Generation 40" au "G40", kundi la wanasiasa wa Zimbabwe wanaomuunga mkono Grace Mugabe.
Hatua wazi ya Bw Mugabe ya kupendelea wanasiasa wa kizazi hiki inaonekana kuwa iliyowakera viongozi wa jeshi, wachanganuzi wanasema.

No comments:

Post a Comment