Rais mpya wa Angola Joao Lourenco amemfuta kazi binti wa mtangulizi wake ambaye amekuwa mkuu wa kampuni ya mafuta ya taifa hilo Sonangol.
Isabel Dos Santos anaaminika kuwa mwanamke tajiri zaidi Afrika.
Babake, Jose Eduardo Dos Santos, alikuwa madarakani kwa miongo minne hadi Septemba mwaka huu.
Bi Dos Santos ni mmoja tu kati ya maafisa wengine wengi ambao wamefutwa kazi na Rais Lourenco.
Aliahidi kukabiliana na ulaji rushwa na wachanganuzi wanasema huenda pengine anataka kudhoofisha ushawishi wa familia ya Dos Santos serikalini.
Angola ndilo taifa la pili kwa uzalishaji wa mafuta lakini uchumi wake umeathiriwa pakubwa na kushuka kwa bei ya mafuta duniani.
No comments:
Post a Comment