Tuesday, November 21

Moto wazuka kituo cha habari cha Clouds Media GroupTanzania

Moshi ukifuka kutoka jengo la Clouds Media Group wakati likiwaka moto
Image captionMoshi ukifuka kutoka jengo la Clouds Media Group wakati likiwaka moto
Jeshi la zima moto limefika katika jengo la kituo cha habari cha Clouds Media Group jijini Dar es salaam, kudhibiti moto uliozuka katika mojawapo ya vyumba vya kurushia matangazo ya televisheni.
Tayari moto umeshadhibitiwa.
Sebastian Maganga, mkuu wa maaudhui na uzalishaji wa Cloud Media Group, ameiambia BBC kwamba, "moto umetokea kati ya saa tatu asubuhi hadi saa nne , athari saizi ni vigumu kuzijua. Eneo ambalo limeungua ni chumba cha kurushia matangazo ya televesheni."
Mojawapo ya wafanyakazi wa Clouds Media Group akijaribu kuokoa baadhi ya vifaa
Image captionMojawapo ya wafanyakazi wa Clouds Media Group akijaribu kuokoa baadhi ya vifaa
Mojowapo ya vipindi vilikuwa vikuruka hewani hapo ambapo moto ulipozuka.
Pia Ambwene Mwakibete, Kaimu Kamanda wa jeshi la zima moto na uokoaji, mkoa wa kipolisi wa Kinondoni, amesema kwamba
"Tumeidhibiti moto ili usimbae kwenye vyumba vingine. Tumeona ni mfumo wa kiyoyozi ambao ni umeme ndio tumeona umeathirika kwa sehemu kubwa."
Matangazo ya kituo hicho yamesitishwa
Image captionMatangazo ya kituo hicho yamesitishwa
Hamna majeruhi wala vifo, na thamani ya uharibifu haijafahamika bado. Chanzo cha moto hadi sasa bado hakijafahamika.
Juhudi za uokoaji wa mali zinaendelea.

No comments:

Post a Comment