Tuesday, November 21

Makamu wa rais aliyefutwa kazi Emmerson Mnangagwa amtaka Mugabe ajiuzulu mara moja

Robert MugabeHaki miliki ya pichaEPA/THE HERALD
Image captionRais Mugabe anakabiliwa na shinikizo kutoka kwa umma na chama chake cha Zanu-PF
Makamu wa rais wa zamani , ambaye kufutwa kwake kazi kulisababisha jeshi kuchukua mamlaka ya nchi , amemtaka rais Robert Mugabe ajiuzulu mara moja.
Emmerson Mnangagwa amesema alitoroka nje ya nchi wiki mbili zilizopita wakati alipobaini kuwa kuna njama za kumuua na hatarejea nchini hadi atakapohakikishiwa usalama wake.
Emmerson MnangagwaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionEmmerson Mnangagwa anatarajiwa kuwa rais ajaye wa Zimbabwe
Chama cha rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kinatarajiwa kuanza mchakato wa kupiga kura ya kutokuwa na imani nae.
Afisa wa Zanu-PF amesema kuwa hoja ya kumnyang'anya urais itawasilishwa bungeni leo Jumanne na mchakato wa kumg'oa madarakani unaweza kuchukua siku mbili tu.
Mashtaka yaliyomo kwenye hoja hiyo ni pamoja na kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 93 "kumpa madaraka makubwa ya kikatiba mkewe Grace, na kushindwa kuheshimu katiba''.
Viongozi wa kijeshi , ambao wiki iliyopita waliingilia kati kuchukua mamlaka ya nchi walisema atakutana na makamu wake wa rais wa zamani aliyeuhamishoni karibuni.
Jeshi limesema kuwa lina mpango na Mugabe kuhusu hali ya baadae.
Mugabe ''alimwachia mkewe mamlaka ya kikatiba
Mugabe ''alimwachia mkewe mamlaka ya kikatiba, licha ya shinikizo kubwa Bwana Mugabe aliwashangaza wengi kwa kukataa kujiuzulu, na badala yake katika hotuma yake kupitia televisheni alisema k

No comments:

Post a Comment