Mkuu huyo wa mkoa huo Godfrey Zambi amemwagiza Katibu tawala wa mkoa huo kuwachukulia hatua watumishi wote wa ofisi yake pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi ambao wamekiuka agizo la Makamu wa Rais.
Ametoa agizo hilo jana Jumamosi baada ya watumishi wa ofisi hizo kutohudhuria mazoezi hayo ambayo alikuwa anayasimamia yeye mwenyewe.
Zambi amesema kitendo cha watumishi hao kutohudhuria mazoezi ni kupuuza agizo la Makamu wa Rais la kutaka kila Jumamosi ya pili ya mwezi watumishi pamoja na wananchi wote kujumuika kwa pamoja na kufanya mazoezi ya viungo.
Katika mazoezi hayo yaliyofanyika kwenye fukwe za bahari ya Lindi mkoani hapo watumishi walioshiriki mazoezi hayo walikuwa 15.
Zambi pia amewapongeza wananchi wa Mkoa wa Lindi kwa kujitokeza kwa wingi katika mazoezi hayo pamoja na kumuunga mkono Makamu wa Rais.
Pia amewaasa wananchi hao kama walivyojitokeza katika mazoezi lakini pia wajitokeze siku ya usafi ambayo hufanyika mwisho wa mwezi.
No comments:
Post a Comment