Akizungumza leo Jumapili, msemaji wa chama hicho, Tumaini Makene amesema haijulikani meya huyo amepelekwa kituo gani na kwa kosa gani.
Amesema Jacob aliapishwa kuwa wakala katika majumuisho ya uchaguzi wa Kata ya Saranga hivyo alikuwa anahusika katika uchaguzi unaoendelea katika kata hiyo.
Makene amesema uongozi wa chama hicho unafuatilia ili kujua sababu za kukamatwa kwake na wapi alipo.
"Sasa kama mtu tunayemtegemea kuwa wakala kwenye majumuisho ya kuhesabu kura unategemea nini, hizi ni rafu ambazo mamlaka husika zinatakiwa kufuatilia," amesema.
No comments:
Post a Comment