Wednesday, November 22

MENEJA WA NYANZA CORMERCIAL FARM APIGWA FAINI YA SH MILIONI 534 AU KIFUNGO CHA MIAKA 20 KWA KUKUTWA NA KUCHA 17 ZA SIMBA


Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemhukumu meneja wa Nyanza Commercial Farm, Dilipkumar Pater, kulipa faini ya Sh milioni 53.4 ama kutumikia kifungo cha miaka 20 jela baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na kucha 17 za simba kinyume na sheria.

Hukumu hiyo imetolewa leo Novemba 22 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama hiyo, Cyprian Mkeha, 

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mkeha alisema ameridhika na ushahidi wa mashahidi wanne uliotolewa upande wa mashtaka na vielelezo vitatu kuwa mshtakiwa kweli alitenda kosa hilo Katika kesi hiyo, mshtakiwa Pater alijitetea mwenyewe.

Hakimu Mkeha amesema mahakama imemuona mshtakiwa Pater ana hatia baada ya upande wa mashtaka kuthibitisha kesi yao pasipo kuacha shaka.

Katika ushahidi, upande wa utetezi waliwasilisha, vielelezo vitatu ambavyo ni kucha za simba, hati ya ukamataji na cheti cha kutathmini kucha hizo.
Kabla ya kusomwa hukumu hiyo, Hakimu Mkeha alimuuliza Wakili wa serikali kama alikuwa na lolote la kusema ndipo, wakili Elia Atanas kwa kushirikiana na wakili Batlida Mushi aliiomba mahakama Kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa watu wengine.

Akijitetea kabla ya kusomewa hukumu hiyo Pater alidai a yeye ni mgonjwa na anategemewa na familia. "Kutokana na ushahidi uliotolewa unaonyesha mshtakiwa alibeba kucha hizo huku akijua ni kosa na akajaribu kuzisafirisha kwenda nchini India kupitia Dubai" amesema Mkeha.

Katika kesi hiyo mshtakiwa huyo anadaiwa kuwa Novemba 19, mwaka 2016, katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Pater alikutwa na kucha 17 za Simba zenye thamani ya Sh 53,483,500 bila ya kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori.

No comments:

Post a Comment