Mwanasiasa nchini Japan amekosolewa na wabunge kwa kujaribu kumleta mtoto wake mchanga katika kikao cha bunge.
Yuka Ogata alisema kuwa alitaka kuonyesha kiwango cha masaibu wanayoyayapitia wanawake wanaofanya kazi na kuwatunza watoto wao wakati mmoja.
Maafisa wa bunge la manispaa ya Kumamoto walisema kuwa alikiuka sheria kwa sababu wageni na waangalizi hawaruhusiwi kuingia ukumbini.
Baada ya mjadala mrefu, Bi Ogata alimuacha mwanae na rafiki yake na kikao kikaanza dakika 40 baadae.
Bunge hilo lilisema kuwa litajadili suala lake kwa ajili ya kuwasaidi wabunge wenye watoto wachanga.
Spika Yoshitomo Sawada aliwaambia waandishi wa habari: "tungependa kufanya kazi katika mfumo ambapo wabunge wanaweza kushiriki katika mikutano pamoja na watoto wao ," liliripoti gazeti la Mainichi.
Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa mbunge Bi Ogata kuhudhuria kikao cha bunge la manispaa cha kawaida tangu alipojifungua mtoto wake wa kiume miezi saba iliyopita.
Aliwaambia waandishi wa habari kuwa aliioma halmashauri ya bunge ama wamruhusu mtoto wake kuwa pamoja nae bungeni ama kumatia huduma ya malezi ya mchana ya mtoto.
"nililitaka bunge kuwa mahala ambapo wanawake wanaowalea watoto wanaweza pia kufanya kazi nzuri ," aliliambia gazeti la Mainichi.
Alisema kitendo chake cha kumleta mwanae bungeni hakikukubalika , lakini akaamua kumle tu mwanae.
No comments:
Post a Comment