Friday, November 24

Hatua ya Rita Ora ya kutunza mayai ya uzazi katika miaka 20 yasifiwa na madaktari

Rita OraHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Rita Ora amefichua kuwa aliweka mayai yake ya uzazi kwenye barafu baada ya miaka 20 alipokuwa akizungumza kwenye kipindi cha Televisheni ya Australia .
Muimbaji huyo wa raia wa Uingereza, ambaye sasa ana umri wa miaka 26 alisemakuwa madaktari walimpenekezea upasuaji wa kuyaondoa mayai hayo mwilini mwake kwasababu " amekuwa akitaka kuwa na familia kubwa".
"Daktari alisema: 'una afya nzuri sasa na itakuwa vema, kwa nini usiyaondoe mayai yako ya uzazi uyatunze , halafu hautakuwa na hofu ya kuwakosa watoto tena ?'," alisema Rita.
Daktari Helen O'Neill, wa chuo kikuu cha London ,anasema: : " Ni bora kuondoa mwilini mwako na kuyatunza mayai yako ya uzazi mapema kuliko kusubiri."
Lakini ni ''hakikisho kamili'' la kupata ujauzuito na wasichana wengi hawawezi kugaramia garama ya upasuaji na utanzaji wa mayai ya uzazi ambayo ni Euro -£5,000 kila mzunguko mmoja wa hedhi.
Daktari O'Neil anasema : "Faida za kuyatunza mayai ya uzazi kwenye barafu ni kwamba unachukua jukumu la kutumga mimba mikononi mwako . Kama ukifanyiwa uchunguzi na ikibainika kwamba una uwezo mdogo wa kutpata ujauzito ni vema kuchukua hatua mapema."
Anasema kuna upungufu mkubwa wa mayai bora ya uzazibaada ya mwanamke kufikia miaka 30 - na kwamba ubora huo huendelea kupungua kadri miaka inavyokwenda.
"Bahati mbaya watu wengi huanza kutunza mayai yao ya uzazi wakiwa na umri wa miaka 35, ambapo wanakuwa wamechelewa kidogo ," alielezea.
Seli za mayai ya uzaziHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Nchini Uingereza , idadi ya wanawake wanaotunza mayai yao ya uzazi kwa ajili ya kupata watoto baadae imeongezeka kwa kiasi kikubwa.
Mwaka 2014, wanawake 816 walitunza mayai yao kwenye barafu kwa ajili ya uzazi wa baadae ilipanda na kufikia hadi asilimia 25% mwaka 2013, kulinga na takwimu za hivi karibuni kutoka mamlaka ya inayofuatilia masuala ya uzazi wa kusaidiwa nchini humo (HFEA).
Hospitali ya wanawake ya London ya mtaa wa Harley, hivi karibuni iliripoti kuwa idadi ya wanawake wanaohudhuria kliniki zake za uzazi wa kusaidiwa fimeongezeka mara tatu kitika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
Kiwango cha uzazi wa kupozesha mayai kwenye friji kilikuwa ni sawa na 14% mwaka 2013, kulingana na mamlaka ya HFEA. Kiwango kilikuwa cha chini kwa wanawake wenye umri wa zaidi ya miaka 38.
Bi Ora anasema alikuwa anatambua tayari kwamba mchakato huo haumaanishi kuwa ana uhakika wa kupata watoto baadae ,alisema : "Nafahamu watu wanaweza kusema , aah! lakini ana umri mdogo '. Nilitaka tu kuchukua tahadhari''.

No comments:

Post a Comment