Polisi ikipiga doria katika mitaa ya Ngagara, kaskazini mwa Bujumbura, Aprili 25, 2015.
Mazungumzo mapya kuhusu mgogoro wa kisiasa wa Burundi yanaanza tena Novemba 27 hadi Desemba 8, kwa mujibu wa timu ya Mwezeshaji katika mgogoro huo, rais wa zamani wa Tanzania, Benjamin Mkapa.
Mazungumzo hayo mapya yatakayo dumu wiki mbili yatakua ni yenye maamuzi, kwa mujibu wa chanzo kilio karibu na timu ya Mwezeshaji.
Mazungumo haya yatadumu siku 13 ili kujaribu kutafuta suluhu ya mgogoro huo uliibuka baada ya rais Pierre Nkurunziza kutangaza nia yake ya kuwania muhula wa tatu wa urais mwaka 2015.
Hii itakua mara ya kwanza serikali ya Burundi kushiri mazungumzo nje ya nchi. Serikali imemtuma Katibu wa kudumu kwenye wizara ya Mambo ya Ndani, Therence Ntahiraja kushiriki mazungumzo hayo. Pia kiongozi wa chama tawala Evariste Ndayishimiye, akiambatana na viongozi wa vyama vya upinzani vinavyounga mkono serikali na mashirika ya kiraia kutoka Bujumbura watakuepo mjini Arusha ili kujaribu kushawishi Mwezeshaji katika mgogoro wa Burundi Benjamin Mkapa na wasaidizi wake kuhamisha mazungumzo hayo nchini Burundi.
Katika mazungumzo yaliyotangulia, serikali ya Burundi ilikataa kushiriki mazungumzo ya moja kwa moja na upinzani wenye msimamo mkali, ulio uhamishoni (Cnared), ikiushtumu kuhusika katika jaribio la mapinduzi lililotibuliwa Mei 14, 2015. Hata hivyo Mwezeshaji rais mstaafu wa Tanzania, Benjamin Mkapa, alikua akijaribu kukutana na kila upande katika mgogoro huo.
Kwa mujibu wa chanzo kilio karibu na timu ya Mwezeshaji, mazungumzo haya huenda yakawa ya mwisho kuhusu mchakato wa amani nchini Burundi
Wiki mbili zilizipita msemaji wake Pancrace Cimpaye, alitangaza kwamba muungano wao hautashiriki mazungumzo hayo, ukishtumu Mwezeshaji katika mazungumzo hayo Benjamin Mkapa kuegemea upande wa serikali na kutaka baada ya mazungumzo hayo mazungumzo mengine kuendelea nchini Burundi.
Cnared itakua na mkutano kabambe hii leo mjini Brussels, nchini Ubelgiji kuwachagua viongozi wake wapya, kwa mujibu wa chanzo rasmi kutoka muungano huo.
Awali mabalozi kutoka nchi mbalimbali za Ulaya na Marekani katika kanda ya Afrika Mashariki wana wasiwasi na uamuzi huo wa timu ya usuluhishi wa kikanda, ambayo imetenga Umoja wa Mataifa, Umoja wa Afrika, na Umoja wa Ulaya katika maandalizi ya mazungumzo hayo ambayo yanaegemea upande wa rais Nkurunziza, kwa mujibu wa baadhi ya mabalozi.
Machafuko nchini Burundi yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 2000 kwa mujibu wa mashirika mablimbali ya haki za binadamu kutoka Burundi n ayale ya kimataifa, na wengine zaidi ya laki tatu kuyahama makazi yao na kukimbilia uhamishoni.
No comments:
Post a Comment