Tangu mwaka 2012, mashirika yasiyo ya kiserikali ya Kirusi na yanayofadhiliwa kimataifa yamelazimika kujiandikisha kama "mawakala wa kigeni." Licha ya unyanyapaa huu, wengi wao wanajikakamua.
Miaka mitano baadaye, DW inalitazama jambo hili kwa makini.
Kwa Marina Koltsova na wenzake, jimbo la Chechnya ni eneo lolote lisiloendeka, eneo tupu kwenye ramani. "Kama jambo la msingi, haturuhusiwi kufanya semina katika kanda ya kaskazini mwa Caucasus, kwa sababu tu tunakabiliwa na unyanyapaa huo," Koltsova, mwanasheria wa shirika la masuala ya haki za binadamu maarufu "Memorial," jijini Moscow aliiambia DW.
"Taasisi za kiserikali katika ngazi zote zimekuwa zinatuambia wazi kwamba tumewekwa kama mawakala wa kigeni - hiyo ina maana wapelelezi - na kwamba hawawezi kushirikiana nasi. Mamlaka zimejulishwa kwa mdomo au hata kwa maandishi," alisema.
Sio tu wanaharakati wa haki za binadamu
Kizuizi hiki ni matokeo ya moja kwa moja ya sheria ambayo ilianza kutumika miaka mitano iliyopita: mnamo 21 Novemba 2012.
Chini ya sheria hiyo, mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yanafanya kazi kisiasa na kupokea fedha kutoka ng'ambo yanatakiwa kujiandikisha kama "mawakala wa kigeni."
Kwa kuongeza, wanatakiwa kufanya hayo hadharani, kwenye tovuti zao, kwa mfano, na lazima wafafanue vyanzo vya fedha zao haraka.
Mashirika ya haki za kibinadamu yanaathirika zaidi, lakini pia mashirika yasiyo ya kiserikali ambayo yanafanya kampeni kwa ajili ya mazingira au masuala ya huduma za afya.
Shirika lisilo la kiserikali la ´Memorial´ liliorodheshwa kwenye regista ya ´mawalaka wa kigeni´ bila ya idhini
Sheria ya "mawakala wa kigeni" ilikuwa moja ya mfululizo wa hatua za kuzuizi ambazo zilianzishwa na serikali ya Kirusi kwa kukabiliana na harakati ya kupinga vuguvugu la upinzani la Kremlin ambalo lilizuka katika kipindi kati ya uchaguzi wa bunge na wa rais wakati wa mwaka 2011/12.
Machoni mwa viongozi wa Kirusi, mashirika yasiyo ya kiserikali ni vyombo vinavyotumiwa na serikali za magharibi kutaka kubadilisha uongozi nchini humo.
Rasmi, Urusi iliteteta hatua yake hii kwa kugusia juu ya sheria ya Marekani juu ya usajili wa mashirika ya nje inayovitaka vyombo vya nje kutoa taarifa za shughuli zao kwa umma.
Wataalamu, hata hivyo, wanazingatia kulinganisha moja kwa moja kati ya vipande viwili vya sheria kuwa na matatizo, kwa sababu nchini Urusi neno "wakala wa kigeni" limehusishwa na ujasusi tangu zama za kisovieti.
Kuharibiwa muonekano ni tatizo kubwa zaidi, alisema Marina Koltsova wa taasisi ya "Memorial," ambayo inafanya kazi kukuza kumbukumbu ya ukandamizaji wa kisiasa katika Muungano wa Sovieti.
Kwa mashirika mengi yasiyokuwa ya kiserikali, sheria hiyo ni kikwazo kikubwa na, hivyo walikataa kujiorodhesha kwa hiari katika orodha ya "wakala wa kigeni" ya Wizara ya Sheria.
Walipata msaada kutoka Baraza la Ulaya, Umoja wa Ulaya na serikali za Magharibi.
Na kulikuwa na upinzani kutoka ndani ya Urusi, pia, kwa mfano kutoka Baraza la Rais la Mashirika ya Kiraia na Haki za Binadamu. Lakini hakuna kilichosaidia.
Hatimaye, Wizara ya Sheria ilifanya jukumu thabiti na kuziorodhesha mashirika yasiokuwa ya kiserikali kwenye rejista ya "mawakala wa kigeni" bila idhini yao.
Miaka mitano sasa, tathmini ya jumla ni mchanganyiko. Baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali, kama Helsinki iliyoko jijini Moscow, kwa mfano, walijiondolea kabisa msaada wa nje ya nchi na wameendelea kuwepo.
Wengine wengi waliwasilisha kesi za kisheria katika mahakama za Kirusi ambazo hazikufaulu - ikiwa ni pamoja na "Memorial", akikumbuka Marina Koltsova: "Mahakama zinaamini kwamba kufanya maonyesho au meza ya mzunguko inapeleka shughuli za kisiasa," alisema.
Memorial ni miongoni mwa mashirika 60 yasiyokuwa ya serikali ambayo yamewasilisha mashtaka na mahakama ya haki za binadamu ya Ulaya huko Strasbourg. Uamuzi unatarajiwa mwishoni mwa mwaka 2018.
No comments:
Post a Comment