Mdee ambaye ni Mbunge wa Kawe anakabiliwa na kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Wakili wa Serikali, Leonard Challo leo Jumatano Novemba 8,2017 amemueleza Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa kuwa kesi hiyo ilipaswa kuanza kusikilizwa lakini shahidi waliyemtarajia ameanza likizo na amesafiri.
Ameiomba Mahakama ipangiwe tarehe nyingine kwa ajili ya kuanza kusikilizwa na kwamba, siku hiyo wataleta shahidi mwingine.
Hakimu Nongwa ameahirisha kesi hiyo hadi Desemba 7,2017 utakapoanza kusikilizwa ushahidi wa upande wa mashtaka.
Aliposomewa maelezo ya awali ya kesi hiyo, Mdee alikumbushwa shtaka linalomkabili, akidaiwa alilitenda Julai 3,2017 makao makuu ya Chadema iliyopo Mtaa wa Ufipa wilayani Kinondoni.
Mdee anadaiwa kumtusi Rais Magufuli kwa kutamka, “Anaongea hovyo hovyo, anatakiwa afungwe breki.”
Kauli hiyo inadaiwa ingeweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Mdee anayetetewa na mawakili Peter Kibatala, Nashon Nkungu, Jeremiah Mtobesya, Faraja Mangula, Omary Msemo na Hekima Mwasipu alifikishwa kwa mara ya kwanza mahakamani Julai 10,2017.
No comments:
Post a Comment