Thursday, November 16

Kunyanyuka na kuanguka kwa Mugabe

Grace Mugabe
Kwa miaka 37, Robert Mugabe alihimili changamoto kwa utawala wake kutoka kwa washirika wake wa zamani, kuanzia upinzani ambao ulikaribia kumuondoa mamlakani katika uchaguzi wa mwaka 2008.
Hivi leo, inaonekana hatimaye amepoteza nguvu yake ya madaraka, hilo limetokea kwa kasi kutokana na vitendo vya mke wake, Grace Mugabe.
Wakati jeshi la Zimbabwe Jumatano lililposema halichukui udhibiti wa serikali, hatua iliyochukua ya kuwaweka chini ya ulinzi kina Mugabe inabainisha ni mara ya kwanza tangu mwaka 1980 rais huyo kutokuwa na mamlaka katika taifa hilo la kusini mwa afrika. ujumbe wa chama tawala katika akaunti ya twitter umesema “si Zimbabwe wala ZANU zinamilikiwa na Mugabe na mke wake.”
Swali juu ya nani atamrithi Mugabe limekuwepo kwa miaka mingi, hasa kama rais, ambaye hivi sasa ana umri wa miaka 93, na anaonekana anazidi kuzeeka na anatumia muda mrefu nchini Singapore kwa likizo na matibabu.
Mugabe amejaribu kukandamiza ushindani ndani ya chama tawala, na chama kilibashiri kwamba rais ataendelea kuwa mwenye afya na mwenye udhibiti. Mwezi Disemba mwaka 2016, chama cha ZANU-PF kilimteua Mugeba kuwa mgombea pekee wa urais kwa uchaguzi wa mwaka 2018.
Hata hivyo ilikuwa vigumu kuficha mapingano ya ndani yaliyokuwa yakijitokeza hadharani. ZANU-PF iligawanyika katika makundi mawili juu ya mapambano ya mrithi wake, kundi moja likimuuna mkono makamu wa rais na mshirika wa Mugabe katika vita vya ukombozi, emerson mnangagwa, na kundi jingine ambalo lilikuwa linamuunga mkono mke wa rais.
Mnangagwa ambaye pia anajulikana kama ‘mamba’, alikuwa mshirika wa karibu wa Mugabe kwa miongo mingi kabla ya ghalfa kufukuzwa kazi hapo novemba 5. Mnangagwa anauungaji mkono mkubwa kutoka kwa wapiganaji vita wa zamani ambao siku zote wamekuwa na mchango mkubwa katika masuala ya Zimbabwe na anaonekana kama nguzo ya uungaji mkono kwa serikali ya Mugabe.
Grace Mugabe mwenye umri wa miaka 52, aliolewa na Mugabe mwaka 1996 baada ya kifo cha mke wake wa kwanza, alikuwa akipendwa na wanaharakati vijana wa ZANI-PF. Kupanda kwake kisiasa katika muda wa miaka minne iliyopita, hata hivyo, hili liliwakasirisha wazimbabwe wengi ambao wanamuona msukumo wake wa uroho wa madaraka.
Watu walishangazwa mwaka 2014 alipopewa shahada ya uzamifu katika sosholojia kutoka chuo kikuu cha zimbawe miezi miwili tu baada ya kujiandikisha chuoni hapo.
Mwaka huo huo, alimkosoa vikali aliyekuwa makamu wa rais kipindi hicho, Joice Mujuru, akisema anapanga njama ya kumuondoa madarakani. Mwezi desemba 2014, Mujuru alifukuzwa kasi kama makamu wa rais na katika uongozi ndani ya chama ZANU-PF.
Mke wa rais alikuwa kwenye vichwa vya habari mwaka 2017, hasa pale aliposema mume wake huenda akawania tena urais, “kama mfu” kama itabidi iwe hivyo. mwezi Agosti, alishutumiwa kwa kumshambulia mwana mitindo mmoja mjini Johannesburg, Afrika Kusini. Mke wa rais alikana vikali shutuma hizo, akisema alikuwa akijaribu akiwalinda watoto wake wa kiume kutoka kwa mwanamke, ambaye alisema alikuwa amelewa.
Nguvu ya mwisho ilikuwa wiki iliyopita pale rais alipomfuta kazi mnangagwa kama makamu wa rais na kupendekeza kuwa mke wake atachukua wadhifa wake na hivyo kumfanya moyo wake kuwa na mapigo ya moyo yaliyodhoofu – akielekea kuondoka katika urais.

No comments:

Post a Comment