Friday, November 3

Keisha atoa ushahidi wenye utata ndoa ya Dogo Janja, Uwoya


Dar es Salaam. Mwanamuziki Keisha amejichanganya kuhusu suala la ndoa kati ya Dogo Janja na mwigizaji, Irene Uwoya akitoa maelezo tofauti kuhusiana na ushiriki wake katika kufanikisha shughuli hiyo.
Awali Keisha akihojiwa mwanzoni mwa kipindi cha Leo Tena cha leo Ijumaa kinachorushwa na kituo cha Redio Clouds amesema alishiriki kumfuata bibi harusi nyumbani kwao baada ya watangazaji kutaka kufahamu kwa nini ndoa haikufungwa huko.
Keisha akimsaidia Dogo Janja kujibu swali hilo alisema: “Nilikuwa mmoja wa waliokwenda nyumbani kwa kina Irene kumfuata kisha tulimpeleka katika eneo la siri ilipofungwa ndoa, unajua mimi ni kama mama au dada mkubwa wa Abdul ( Dogo Janja) kwa sababu Madee ni kama baba yake asingweza kwenda peke yake.”
Lakini watangazaji walipoendelea na mahojiano Keisha alibadilisha kauli yake akisema hata yeye hakuwa akifahamu anayeolewa ni nani na pia hakuamini iwapo ni tukio la kweli mpaka aliposhuhudia tendo zima.
“Nilipofika nilimuuliza Johari (mwigizaji) ambaye alikuwa mmoja wa mashahidi iwapo ni ndoa kweli na siyo filamu. Johari alisema siwezi kukudanganya hii ndoa kweli. Mimi nimeolewa kwa hiyo niliposhuhudia tukio zima nikajiridhisha kuwa ile ndoa haswa,” amesema Keisha.

No comments:

Post a Comment