Wednesday, November 29

Donald Trump asambaza video za 'waeneza chuki'

Donald TrumpHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Donald Trump amesambaza video mbili kutoka kwa kundi la mrengo wa kulia la Uingereza ambazo zinaeneza chuki.
Ujumbe wa kwanza umekuwa wa Jayda Fransen, naibu kiongozi wa kundi la Britain First, ambao una video inayodai kuonyesha mhamiaji Mwislamu akimshambulia mwanamume ambaye anatumia magongo kutembea.
Amesambaza pia video nyingine mbili za watu ambao Bi Fransen anadai ni Waislamu.
Britain First ni kundi lililoanzishwa mwaka 2011 na waliokuwa wanachama wa chama cha mrengo wa kulia cha Uingereza cha British National Party (BNP).
Kundi hilo limekuwa likiwavutia watu mitandao ya kijamii kwa ujumbe wa utata dhidi ya kile ambacho wanasema ni "Kusilimishwa kwa Uingereza".
Kundi hilo limewadhamini wafuasi wake kuwania katika uchaguzi na uchaguzi mdogo Ulaya na wakivumisha sera za kupinga wahamiaji na utoaji wa mimba. Lakini hakijashinda hata kiti kimoja.
Kundi hilo liliwania katika uchaguzi wa majuzi wa umeya London, ambapo kilipata 1.2% ya kura.
Video ya kwanza kabisa ilikuwa imesambazwa na mchanganuzi mhafidhina wa masuala mbalimbali Marekani Ann Coulter ambaye hufuatwa na Trump kwenye Twitter.
Bi Fransen ana zaidi ya wafuasi 52,000 kwenye Twitter.
The tweets shared on Trump's timelineHaki miliki ya pichaTWITTER/@REALDONALDTRUMP
Image captionThe tweets were flagged as containing sensitive material by Twitter
Mwanamke huyo amejibu kwa furaha hatua ya Trump kueneza ujumbe wake.
Ameandika kwenye ukurasa wake: "Donald Trump mwenyewe amesambaza video hizi na ana karibu wafuasi 44 milioni."
"Mungu akubariki Trump! Mungu aibariki Marekani!" ameongeza.
Ujumbe huo pia umesambazwa katika ukurasa wa Twitter wa Britain First.
Deputy leader of Britain First Jayda FransenHaki miliki ya pichaPA
Image captionJayda Fransen ana zaidi ya wafuasi 52,000 Twitter
Mapema mwezi huu, Bi Fransen alishtakiwa kwa kutumia "lugha au tabia ya matusi au ya kutishia" wakati wa hotuba alizozitoa Belfast.
Atafika kortini katika Mahakama ya Hakimu Belfast Alhamisi 14 Desemba.
Uamuzi wa Bw Trump wa kusambaza video hiyo umeonekana kuwashangaza wengi katika mitandao ya kijamii.

No comments:

Post a Comment