Akizindua mpango huo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, aliishukuru BancABC kwa kushirikiana na Hospitali ya Muhimbili katika suala hilo la kutoa huduma ya bima ya afya kwa watoto.
Alisema mradi huo kushirikiana na BancABC unaendea sambamba na malengo ya serikali iliyojiwekea katika kuhakikisha kuwa jamii inapata huduma za afya kwa uhakika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwani watoto ndio moja ya makundi ambayo huathirika sana wasipopatiwa huduma za Afya za uhakika.
“Natoa wito kwa wazazi watumie fursa hii iliyotolewa na BancABC kwa ushirikiano na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa kuwafungulia watoto wao akaunti BancABC ili kuhakikisha watoto wao wanapata huduma kwa uhakika muda wowote bila ya ulazima wa kuwa na fedha tasilimu pale mtoto anapougua,” amesema.
Aidha, ametoa wito kwa watoa huduma za kifedha nchini pamoja na mashirika mengine kuhakikisha yanaiga mfano wa BancABC kwani wizara yake iko tayari kushirikiana na taasisi ambazo ziko tayari kuimaisha huduma katika sekta ya afya hasa upande wa utoaji huduma.
Naye Mkuu wa Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo na wafanyabiashara wa kati wa benki hiyo, Joyce Malai, amesema BancABC inatambua umuhimu wa kuwa kampuni inayowajibika katika masuala ya kijamii kwa kurudisha kwa jamii sehemu ya faida na hasa katika sekta muhimu sana ya afya.
Amebainisha kuwa dhamira hii ya BancABC kusaidia kuimarisha huduma za jamii hasa kupitia kuwezesha afya ya watoto ni ya msingi sana kwa kuwa pia inasaidia serikali kufikia malengo yake.
Amesema baada ya kufungua akaunti hizo, wazazi wa watoto wenye akaunti hizo watakuwa wanahimizwa wakewe fedha mara kwa mara kwa ajili ya bima ya watoto wao ili wapate huduma kupitia akaunti hizo za Mwangaza Junior Kids Account ambayo haina tozo ya kila mwezi.
Huduma hiyo ya bima haitakuwa na masharti kuhusu umri.
“Wazazi wanaweza kufungua akaunti kwa mtoto zaidi ya mmoja na kuweka fedha kiasi chochote wanachotaka kwani itasaidia kuhakikisha watoto wao wana bima,” amesema.
Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof Lawrence Museru, ameishukuru BancABC kwa ushirikiano huo na kusema hatua hii haitasaidia tu watoto kupata huduma za afya kwa kupitia bima, bali itawajengea pia utamaduni wa kuweka akiba katika benki kuanzia utotoni.
“Kwa sasa akaunti hizi zitafunguliwa na wazazi wao ila watakuwa wakitambua umuhimu wa huduma hii na wataendelea nayo hadi ukubwani," amesema na kutoa rai kwa wazazi watumie fursa hiyo vizuri.
No comments:
Post a Comment