Sunday, October 15

Zuma atakiwa kujibu mashtaka ya rushwa Afrika Kusini

Jacob ZumaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionJacob Zuma amekanusha tuhuma zote dhidi yake
Mahakama nchini Afrika Kusini imetupilia mbali rufaa iliyokuwa imewasilishwa na Rais Jacob Zuma kupinga kufufuliwa kwa mashtaka ya ulaji rushwa dhidi yake.
Bw Zuma na maafisa wengine wakuu serikali walikuwa wametuhumiwa kupokea mlungula wakati wa ununuzi wa ndege za kivita, maboti ya kushika doria na silaha nyingine.
Kuna jumla ya mashtaka 783 kuhusiana na mkataba huo wa mwaka 1999 wa ununuzi wa silaha za mamilioni ya dola.
Mashtaka hayo yaliwasilishwa mara ya kwanza dhidi ya Bw Zuma mwaka 2005 lakini yakaondolewa na waendesha mashtaka mwaka 2009 na kumuwezesha Bw Zuma kuwania urais.
Hata hivyo, mwaka jana, Mahakama Kuu mjini Pretoria iliamua kwamba kiongozi huyo anafaa kujibu mashtaka hayo.
Bw Zuma baadaye aliwasilisha rufaa katika Mahakama ya Juu ya Rufaa kupinga hatua ya kufufuliwa kwa mashtaka hayo.
Rais huyo amekuwa akisisitiza kwamba hana hatia.
Mashtaka hayo yanahusiana na uhusiano kati ya Zuma na mfanyabiashara Shabir Shaik aliyepatikana na hatua mwaka 2005 ya kupokea rushwa kutoka kwa kampuni ya uuzani wa silaha ya Ufaransa "kwa niaba ya Zuma".
Demonstrators protesting against the South African president and calling for his resignation hold placards and shout slogans outside the Gupta Family compound in Johannesburg on April 7, 2017.Haki miliki ya pichaAFP
Muhula wa sasa wa Rais Zuma utafikia kikomo 2019 na hataweza kuwania tena kwani ameongoza kwa mihula miwili.
Katika kipindi ambacho amekuwa madarakani, amekabiliwa na kura ya kutokuwa na imani naye mara nane, na kunusurika.
Ndiye rais aliyenusurika majaribio mengi zaidi ya kutaka kumuondoa madarakani Afrika Kusini tangu kumalizika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi mwaka 1994.

No comments:

Post a Comment