Majimbo 18 ya Marekani yamesema kuwa yataupeleka utawala wa Rais Trump mahakamani iwapo utaendelea na mpango wake wa kukataa kulipia bima ya afya ya malipo ya kadri ujulikanao kama Obamacare.
Bwana Trump anasema kuwa hataki kampuni kama hizo za Bima kutajirika na akasisitiza kuwa malipo hayo ya Bima ni kinyume cha sheria.
Lakini wakosoaji wanasema kuwa malipo ya bima yatapanda.
Juhudi za Rais Trump kufutilia mbali bima hiyo ya malipo nafuu zimepingwa vikali na Wabunge wa Congress, kukiwemo wanachama wa chama chake cha Republican.
No comments:
Post a Comment