Kila mtu amekuwa akidhania kwamba uhusiano wa wapenzi maarufu Afrika Mashariki na kati msanii wa bongo fleva Diamond Platinumz na mfanyibiashara wa Uganda Zari Hassan ulikuwa umevunjika baada ya kashfa ya Diamond iliomuhusisha na mwanamitindo Hamisa Mobeto.
Zari yeye mwenyewe amjitokeza na kushutumu uvumi huo ambao umekuwa ukisambaa katika mitandao ya blogi, kufuatia hatua yake ya kuondoa picha za Diamond katika mitandao yake mbali na kutohudhuria sherehe ya kuzaliwa kwake.
Inadaiwa hata kadi ya siku ya kuzaliwa hakumtumia mpenziwe na baba ya watoto wake wawili Diamond Platinumz.
Wakati Diamond alipokiri kuwa na uhusiano mwengine nje na Hamisa na kupata mtoto naye , ilikuwa mwanzo wa vita vya mitandaoni kati ya wapenzi hao wawili na kuzua uvumi kwamba huenda wataachana.
Hatahivyo akizungumza kwa mara ya kwanza kuhusu kisa hicho Zari amethibitisha kwamba bado yuko na mpenziwe Diamond na kile wanachojaribu kufanya ni kutoweka hadharani maisha yao huku wakiendelea kushauriana.
Alisema: Nilimtakia siku njema ya kuzaliwa lakini sio hadharani bali katika mtandao wa Whatsup.Tunajaribu kuondoa maisha yetu ya kibinafsi katika mitandao ya kijamii.Na kila tunapoendelea kujiondoa katika mitandao ya kijamii ndio tunazidi kupata uvumi, lakini hakuna tatizo kama hilo kila kitu kiko shwari, Zari alisema katika mahijiano na idhaa moja maarufu ya Tanzania.
Habari za penzi lao kuisha zilizusha madai kwamba hatua hiyo itaathiri mikataba ya mamilioni ya fedha waliotia saini ikiwemo kampuni kadhaa.
No comments:
Post a Comment