Sunday, October 15

Obama na Michelle washangazwa na tuhuma zinazomkabili Harvey Weinstein

Harvey Weinstein ni mwandaaji filamu maarufuHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionHarvey Weinstein ni mwandaaji filamu maarufu
Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama, na mkewe, Michelle, wamesema wameshangazwa sana na tuhuma za udhalilishaji wa kimapenzi wa wanawake ambazo zinamkabili mwandaaji wa filamu wa Hollywood Harvey Weinstein.
Bw Weinstein alikuwa anachanga fedha nyingi kwa chama cha Democratic.
Kampuni yake ilimfuta kazi Jumapili kutokana na tuhuma hizo.
Binti wa rais huyo wa zamani, Malia, alifanya kazi kama mkurufunzi katika kampuni ya Weinstein majira yaliyopita ya joto.
Mwandaaji huyo wa filamu ametuhumiwa kuwabaka wanawake watatu.
Baadhi ya waigizaji nyota Hollywood wamejitokeza na kudai kwamba walidhalilishwa kingono pia ni Weinstein wakiwemo Angelina Jolie, Mira Sorvino na Gwyneth Paltrow.
Produsa huyo amekanusha tuhuma hizo na kusema kwamba alishiriki tendo la ngono na wanawake hao kwa hiari yao.
Angelina Jolie (kushoto) na Gwyneth Paltrow ni miongoni mwa waliomtuhumu WeinsteinHaki miliki ya pichaPA
Image captionAngelina Jolie (kushoto) na Gwyneth Paltrow ni miongoni mwa waliomtuhumu Weinstein
Mke wake Georgina Chapman ametangaza kwamba atamwacha.
Chapman, 41, ambaye ni mwanzilishi mwenza wa kampuni ya mitindo ya mavazi ya Marchesa, na Weinstein, 65, wana watoto wawili.
Jolie aliandika kwenye barua pepe: "Nilikuwa na kisa cha kusikitisha sana kati yangu na Harvey Weinstein wakati wa ujana wangu, na kwa sababu yake, niliamua kwamba singefanya kazi naye tena na nilikuwa nikiwatahadharisha wengine wakifanya kazi naye.
"Tabia hii dhidi ya wanawake katika fani yoyote haikubaliki katika taifa lolote lile."

No comments:

Post a Comment