Mpango huo umebainishwa na Mkurugenzi mpya wa kampuni hiyo, Sherif Barbary alipokuwa akijitambulisha kwa vyombo vya habari jijini hapa.
“Tunataka tuwe kampuni ya Afrika Mashariki. Kutoka kwenye mkongo wa Taifa tunahudumia kampuni nyingi nchini ingawa tunao uwezo wa kuziunganisha nchi zote za maziwa makuu,” alisema Barbary.
Alisema utekelezaji wa mpango huo utaongeza mapato ya kampuni hiyo na kusaidia kukuza pato la Taifa kwa kuwa matumizi ya intaneti yanaongezeka kila siku duniani yakichangiwa na kasi ya maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Katika kufanikisha lengo la kutoa intaneti bora zaidi, alisema kampuni hiyo inaajiri wataalamu pamoja na kufanya kazi na kampuni zenye ujuzi wa juu kwa ajili ya kurahisisha maisha ya kidijitali nchini.
Kati ya Aprili mpaka Juni, taarifa za Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) zinaonyesha watumiaji wa mtandao huo wamepungua kutoka 1,004,967 mpaka 987,848 hivyo kuziweka juu kampuni za Smart na Halotel kwa wingi huo.
Ndani ya kipindi hicho, wateja wa Zantel wa huduma za fedha kupitia EasyPesa waliongezeka kutoka 213,660 mpaka 246,417.
Akieleza mpango wake kwenye hilo, Barbary alisema kwamba kampuni hiyo inaimarisha miundombinu kwanza.
Alisema kwamba licha ya kuangalia namna ya kufanikisha huduma hiyo bila kukwaza utamaduni wa jamii husika, Zantel pia inaangalia namna ya kushirikiana na ofisi za umma ili kurahisisha malipo.
“Namna pekee ya kutengeneza fedha ni kumridhisha mteja. Zanzibar kuna Waislamu wengi, hivyo tunatoa huduma za Kiislamu ili kuendana na mahitaji yao,” alisema bosi huyo ambaye ni raia wa Misri.
Mteja wa Zantel, Yacoub Rahim aliutaka uongozi mpya wa kampuni hiyo kuongeza idadi ya wateja pamoja na kurahisisha zaidi mawasiliano inayotoa kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment