Zaidi ya watu 50 wameuawa na takriban 200 kujeruhiwa kwenye ufyatuaji wa risasi wakati wa tamasha la muziki huko Las Vegas, Marekani.
Mtu mwenye bunduki mwenye umri wa maiak 64 Stephen Paddock aliafyatua risasi kutoka ghoroga ya 32 kwenye hoteli ya Mandalay Bay, kwenda kwa tamasha lililokuwa likiendelea nje.
Polisi wanasema mshukiwa ambaye alitajwa kuwa makaazi wa mji huo na ambaye hakutajwa jina ameuawa.
Mamia ya watu walikimbia eneo hilo na milio ya risasi ikasikika kwa muda kwenye video zilizochapishwa katika mitandao ya kijamii.
Ufyatuaji huo ulitokea mwendo wa saa 05:30 GMT na walioshuhudia walisema kuwa mamia ya risasi zilifyatuliwa.
Usafiri wa ndege ulisitishwa kutoka uwanja wa ndege wa McCarran mjini Las Vegas
No comments:
Post a Comment