BBC itazindua matangazo yake kwa lugha mpya nne nchini India.
Uzinduzi huo ni sehemu ya upanuzi mkubwa zaidi kuwai kufanywa na BBC tangu miaka ya 1940, kufuatia ufadhili wa serikali uliotangazwa mwaka 2016.
BBC kwa sasa inatangaza kwa lugha 40.
Lugha hizo mpya za India ni pamoja na Marathi, Gujarati, Telugu and Punjabi.
Mitandao mipya ya lugha inazinduliwa leo.
Haya ni baadhi ya mambo kuhusu sehemu ambapo lugha hizo zinazinduliwa:
Maharashtra:
Lugha: Marathi, inayozungumzwa na takriban watu milioni 73
Eneo: Magharibi mwa India
Umaarufuwake: Jimbo tajiri zaid nchini India, Mumbai na Bollywood
Gujarat:
Lugha: Gujarati, inayozungumzwa na watu milioni 50
Eneo: Magharibi mwa India
Umaarufu wake: Vyakula vua mboga mboga , ujuzi mkubwa wa biashara na densi ya dandiya
Punjab:
Lugha: Punjabi, inayozungumzwa na watu milioni 100 lugha namba 11 inayotumiwa zaidi duniani
Eneo: Kaskazini magharibi mwa India
Umaarufu wake: Kilimo, Bhangra, na hekalu la dhahabu
Andhra Pradesh na Telangana:
Lugha: Telugu, inayozungumzwa na watu milioni 75
Eneo: Kusini mwa India
Umaarufu: Tirupati - hekalu tajiri zaidi duniani na Hyderabadi Biryani, muskiti wa karne ya 16th
No comments:
Post a Comment