Wednesday, October 4

Yahoo yasema udukuzi wa mwaka 2013 uliathiri akaunti zote bilioni 3

Yahoo logo on a smartphoneHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionYahoo yasema udukuzi wa mwaka 2013 uliathiri akaunti zote bilioni 3
Yahoo imesema kuwa akaunti zote bilioni 3 za wateja zilidukuliwa mwaka 2013.
Kampuni hiyo iliyonunuliwa na Verizon mwaka huu ilisema uchunguzi ulionyesha kwa udukuzi huo ulikuwa mkubwa kuliko ilivyofikiriwa awali.
Hata hivyo taarifa zilizoibwa hazikujumuisha za benki.
Awali Yahoo ilikuwa imesema kuwa zaidi ya akaunti bilioni moja zilikuwa zimedukuliwa.
Huku Yahoo ikisema kuwa tangazo hilo la hivi punde sio tisho mpya usalala wake, inatuma barua pepe kwa watumiaji wapya waliiathiriwa.
Yahoo ilinunuliwa na kampuni kubwa ya mawasiliano ya Marekani Verizon, katika mchakato uliokamilika mwaka 2013 Juni.
Maafikiano hayo yalitangazwa mwaka uliopita wakati kanpuni hiyo yenye matatizo ilikubali kuuza biashara yake kuu ya mtandoa kwa Verizon kwa dola bilioni 4.8.
Hata hivyo pesa hizo zilishuka hadi dola bilioni 4.5 wakati Yahoo ilitangaza kuwa ilikuwa muathiriwa wa udukuzi mkubwa wa mwaka 2013 na 2014.

No comments:

Post a Comment