Tuesday, October 31

White House yajitenga na mashtaka ya Mueller kuhusu uchunguzi wa Rashia

Paul Manafort akipita mbele ya wapiga picha akitoka Mahakama ya Serikali kuu mjini Washington, Oct. 30, 2017.
Ikulu ya Marekani imechukua msimamo wa kujitetea na kumtenganisha Rais Donald Trump na mashtaka yaliyofunguliwa dhidi ya washauri wa zamani wa kampeni yake na mwendesha mashtaka maalum Robert Mueller siku ya Jumatatu.
Mashtaka hayo yanahusiana na uchunguzi anayofanya Mueller kutaka kujua ikiwa Rashia ilijaribu kushawishi uchaguzi wa rais wa mwaka 2016.
Picha iliyochorwa mahakamani ya Manafort na mshirika wake, Rick Gates, mahakamani Washington, Oct. 30, 2017
Picha iliyochorwa mahakamani ya Manafort na mshirika wake, Rick Gates, mahakamani Washington, Oct. 30, 2017
Washauri hao wawili, mwenyekiti wa zamani wa kampeni ya Paul Manafort na mshirika wake wa biashara wa muda mrefu Rick Gates, wametajwa katika mashtaka 12 kuhusiana na kuhalalisha fedha zilizopatikana kwa njia ya haramu, kukwepa kulipa kodi, kujaribu kuihujumu Marekani na mashtaka mengine. Wote wamedai hawana hatia mbele ya Mahakama ya serikali kuu mjini Washington.
Profesa Julius Nyang'oro mchambuzi wa masuala ya kisiasa
Profesa Julius Nyang'oro mchambuzi wa masuala ya kisiasa
Akizungumza na Sauti ya Amerika Profesa Julius Nyang'oro amesema kufunguliwa mashtaka washauri hao waandamizi wa zamani inamaanisha uchunguzi unaonesha unapata ushahidi kwamba huwenda Rashia ilijihusisha kushawishi watu kumchagua Trump, lakini anasema "sasa suala tunaojiuliza, je huo uhusiano ulikua ambao ni uhusiano unashika misingi ya uchaguzi wa Marekani ndio au hapana."
Nyang'oro anasema lengo kuu la Mueller ni kumsikiliza Donald Trump, kwa hivyo akianza kuwasaka maafisa wachini hadi kuwakaribia wakubwa na wale wote waliokua katika kampeni yake basi lazima kuna wale watakaoanza kuzungumza na hivyo ataweza kumfikia Trump na hapo kuweza kujua ukweli wa mambo.

No comments:

Post a Comment