Na Agness Francis ,Blogu ya jamii
Waziri wa habari,utamaduni, sanaa na michezo, Dkt Harrison Mwakyembe amehudhudhuria mkutano wa wasanii wa shirikisho la sanaa za ufundi hapa nchini kusikiliza maendeleo na changamoto zinazowakabili wasanii hao na kuwataka kuchangamkia fursa kazi za mikono yao.
Katika mkutano huo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, Shirikisho hilo la sanaa za ufundi hapa nchini ambalo lilianza rasmi mwaka 2009 na kupata usajili wake mwaka 2010 ambapo wasanii hao walimepata mafanikio kwa kushirikiana na (BASATA)pamoja na ubalozi wa China katika mradi ambao ulijulikana kwa jina la Tingatinga Art Biennale na walipatikana washindi wawili ambao walizawadiwa tiketi ya kwenda nchini China.
Vile vile shirikisho limeeleza changamoto zinazowakabili wasanii hao kuwa Elimu ya sanaa za ufundi haifundishwi mashuleni, hakuna kituo maalumu cha Taifa cha kuonesha kazi za wasanii na masoko ya sanaa kuwa hafifu kutokana na ugumu wa usafirishaji wa vinyago kwenda nje ya nchi kupitia uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere.
Aidha Waziri Mwakyembe amekanusha dhana potofu isemwayo kuwa wasanii wa sanaa za ufundi wengi wao hawajaenda shule na amesema kuwa wizara yake itaunga mkono na kushirikiana bega kwa bega na juhudi za sanaa hiyo ili kuepukana na wanyonyaji wa kazi ya wasanii hao.
Nae naibu waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo Juliana Shonza amemalizia kwa kutoa wito kwa Baraza la sanaa la Taifa (BASATA) kuendelea kuinua vipaji kwa kuweza kuwafikia hasa wasanii wa mikoani na wilayani ambao wamesahaulika kwa muda mrefu katika kuiendeleza tasni hiyo.
Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo, Dkt Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wasanii wa shirikisho la sanaa za ufundi Tanzania pamoja kuwapongeza kwa kazi za mikoni wanazozifanya wasanii hao leo katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam.
Naibu waziri wa habari,utamaduni,sanaa na michezo Juliana Shonza, akizungumza na wandishi wa habari pamoja na wasanii wa shirikisho la sanaa za ufundi Tanzania na kuwataka( BASATA) kuendelea kuinua vipaji vya wasanii hapa nchini hasa kwa wale walioko wa mikoani.
Wageni waalikwa waliojitokeza kwa wingi katika kuhudhuria mkutano uliofanyika leo katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam.
Wasanii wa maigizo ya maonyesho ya jukwaani wakifanya igizo linalohusu kampeni ya kuzuia rushwa leo katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment