Monday, October 2

Watu 2 wauawa kwenye shambulizi la kisu Ufaransa

Police stand on the steps leading to Marseille train stationHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWatu 2 wauawa kwenye shambulizi la kisu Ufaransa
Watu wawili wameuawa kwenye shambulizi la kisu katika kituo cha treni cha Saint Charles huko Marseille nchini Ufaransa, kwa mujibu wa vyombo vya habari.
Mshambuliaji aliuawa na maafisa wa usalama kwenye mji huo ulio Kusini mwa Ufaransa.
Waziri wa mashauri ya ndani nchini Ufaransa, GĂ©rard Collomb, anasema anaelekea eneo hilo.
Polisi waliandika katika mtandao wa twitter kuwa hali imethibitishwa na mshambuliaji kuuliwa.
Afisa mmoja wa polisi ambaye hakutajwa jina aliliambia gazeti la Le Monde kuwa mshambuliaji alitamka maneno "Allahu akbar".
This file photo taken on December 10, 2007 shows the Saint-Charles train station in Marseille.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionKisa hicho kilitokea katika kituo cha treni cha St Charles Marseille

No comments:

Post a Comment