Monday, October 2

Rais Trump ataka viongozi wake watulie

Marekani
Image captionRais wa Marekani Donald Trump
Rais w Marekani Donald Trump amemwambia waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo , Rex Tillerson, asipoteze muda wake kufanya majadiliano ya kusitisha majaribio na utumizi wa sialaha za nyuklia na kiongozi wa Korea Kaskazini.
Mwisahoni mwa juma lililopita bwana Tillerson alibainisha kwamba Marekani ilikuwa ya mawasiliano ya moja kwa moja na Korea ya Kaskazin kuhusu mipango yake ya nyuklia na kombora.
Lakini, akimaanisha Kim Jong Un kama 'mtu mdogo wa roketi', Rais Trump alitupia kitu kwenye mojawapo ya mitandao ya kijamii anayotumia kwamba waziri wake Tillerson anapaswa kuhifadhi nguvu zake badala ya kuzipoteza bure.
Ofisa mmoja wa Marekani baadaye aliiambia shirika la habari la Reuters kwamba rais haamini kwamba sasa ni wakati muafaka wa kujadiliana na Korea ya Kaskazini, kutokana na "mashambulizi" yake.
Ofisa huyo alisema njia yoyote ya kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili ilitumika kujaribu kupata uhuru wa Wamarekani waliofungwa na Korea ya Kaskazini

No comments:

Post a Comment