Wagombea katika uchaguzi huo uliofanyika leo Alhamisi kwenye Uwanja wa Sokoine jijini hapa ni Afrey Nsomba, Ackim Mwakalindile na Edeni Katininda.
Mgombea wa kwanza kujinadi alikuwa Katininda aliyesema CCM Mbeya Mjini ina tatizo moja kubwa la kulikomboa jimbo na Halmashauri ya Jiji la Mbeya, hivyo aliwaomba wapiga kura wamchague kwa kuwa ana uwezo wa kuhakikisha linarudi mikononi mwa CCM.
“Ninajua fika Mbeya Mjini pana tatizo kubwa, ni namna ya kulikomba jimbo letu… mimi na ninyi tutalikomboa ndiyo maana nimekuja mbele yenu, tumeteswa kwa muda mrefu, sasa ni wakati wetu kushika jimbo na viti vyote vya madiwani,” amesema.
Mgombea mwingine, Mwakalindile aliwaomba wapiga kura kumchagua mtu makini atakayeweza kuhakikisha jimbo linakombolewa kwa kuwa ni aibu kuona jimbo na halmashauri vipo upinzani.
“Nawaomba tumchague mtu makini atakayeweza kukomboa jimbo na viti vyote vya udiwani, ndugu zangu ni aibu sana na nazungumza haya kwa uchungu. Tuache ukabila, tuache malumbano, tuache siasa zisizo na tija. Naomba kura zenu kazi hii ninaiweza,” amesema.
Mgombea Nsomba amesema kiu ya CCM Mbeya Mjini ni kulikomba jimbo, hivyo aliwaahidi wapiga kura wakimchagua atashirikiana na wanachama wote kutwaa jimbo na halmashauri.
Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 CCM Mbeya Mjini ilishindwa kumng’oa Sugu lakini ilijikuta ikipoteza viti vingi vya udiwani, hivyo Chadema kunyakua halmashauri ya jiji hilo kwa kuwa na viti 26 vya udiwani dhidi ya 10 vya CCM.
Kwa mujibu wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kati ya wabunge 257 waliochanguliwa na wapiga kura, Sugu aliongoza kwa wingi wa kura alizopata.
Sugu alipata kura 108,566 kati ya 166,256 zilizopigwa akiwaacha wapinzani wake wakigawana kura 57,690.
No comments:
Post a Comment