Tuesday, October 17

Wadukuzi wa Korea Kaskazini wadukua kampuni ya televisheni Uingereza

Kim Jong-unHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMaafisa wa Korea Kaskazini walijibu kwa hasira wakati taarifa kuhusu kipindi hicho zilifichuka mara ya kwanza.
Wadukuzi wa Korea Kaskazini wamelenga kampuni moja ya vipindi televisheni nchini Uingereza ambayo inatengeneza kipindi wa kuigiza kuhusu nchi hiyo.
Kipindi hicho ambacho kilitarajiwa kuandikwa na mwandishi ambaye ashateuliwa kuwania tuzo za Oscar sasa kimesitishwa.
Mwezi Agosti mwaka 2014 Channel 4 ilitangaza kuwa kipindi hicho kitakuwa kipya na cha kuchokoza.
Kipindi hicho kinachojulikana kama Opposite Number, kinahusu mwanasayansi ya nyuklia muingereza ambaye amefungwa nchini Korea Kaskazini.
Kompiuta za kampuni husika za Mammoth Screen zilidukuliwa.
Mradi huo haujapiga hatua kutokana na kushindwa kupata ufadhili kwa mujibu wa kampuni hiyo.
Maafisa wa Korea Kaskazini walijibu kwa hasira wakati taarifa kuhusu kipindi hicho zilifichuka mara ya kwanza.
Matt CharmanHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMwandishi wa Opposite Number Matt Charman
Pyongyang ilitoa wito kwa serikali ya Uingereza kuzima kipindi hicho ili kuzuia kuharibu uhusiano.
Korea Kaskazini kisha ikachukua hatua zaidi na kudukua kompiuta za kampuni husika.
Udukuzi huo haukusababisha uharibifu lakini, kuhusika kwa wadukuzi wa Korea Kaskazini mitandaoni kulizua hofu juu ya ni kipi wana uwezo wa kukifanya.
Hofu hiyo ilitokana sababu Sony Pictures ililengwa na udukuzi kama huo mwezi Novemba mwaka 2014.
Marekani ilisema kuwa udukuzi huo uliendeshwa na Korea Kaskazini.
Udukuzi huo nao ulikuwa ni jibu kwa filamu iliyopangwa kutolewa kwa jina The Interview, mchezo ambao kiongozi wa Korea Kaskazini aliuawa.
The InterviewHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionFilamu ya Sony The Interview ilitupiliwa mbali baada ya kudukuliwa

No comments:

Post a Comment