Vishoka ni mafundi wa umeme ambao hujifanya waajiriwa wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na kutoa huduma zote zinazotakiwa.
Na ndivyo walivyofanya katika vijiji vya Ilalabwe na Logombo vilivyopo Kata ya Iponjoli ambako wakazi walishaanza kutumia nishati hiyo kabla ya Tanesco kubaini na kwenda kung’oa miundombinu hiyo.
Vishoka hao walivamia mradi wa Rea ambao ulikuwa haujakamilika na kuwaunganishia umeme wakazi kwa kutumia nguzo zilizoibwa na mita ambazo hazimo kwenye mfumo wa Tanesco.
Baada ya kubaini, meneja wa Tanesco Mkoa wa Mbeya, Benedict Bahati alisema ofisi yake ilitumia polisi kwenda kung’oa miundombinu ya nishati hiyo katika vijiji hivyo baada ya kubaini kuwa nguzo zilizofungwa ziliibwa, wakati mita zilizofungwa kwenye nyumba za wananchi hazipo kwenye mfumo wake.
Sakata hilo lilitokea Septemba 13 katika eneo ambalo Serikali ilikuwa ikitekeleza awamu ya pili ya mradi wa Rea na Bahati alisema kuna kampuni iliyopewa zabuni ya kusambaza umeme katika Kata ya Iponjola, lakini haikuendelea kutokana na sababu ambazo hakuzitaja.
Alisema wakati hilo likifanyika, kuna vijiji vingine vilikuwa vimeshaunganishiwa umeme na baadhi vilikuwa bado na ndivyo ambavyo baadaye viliunganishiwa kinyemela.
Alisema tukio hilo la aina yake lilibainika baada ya kampuni za Stage International Constructor na Suma Hydro zilizopewa zabuni na Rea kulalamika kwamba kuna nguzo zimeibwa.
“Ndipo msako ukaanza na kubaini zimefungwa katika vijiji vile. Pia tulibaini mita zilizofungwa si mali ya Tanesco kwa kuwa zina tofauti ya namba za siri na hata mwonekano,” alisema.
Alisema walianza kung’oa miundombinu wakati polisi wakiendelea na utaratibu wa uchunguzi ili kubaini aliyewafungia umeme wananchi hao.
Alisema waling’oa nguzo 57 ambazo zilibainika ziliibwa kutoka kampuni moja inayoendelea na usambazaji umeme wa Rea wilayani Rungwe. Pia waling’oa mita 17 ambazo zilikuwa zimefungwa na kufanya kazi katika nyumba 17.
Suala hilo limewafanya wananchi wa vijiji vya Ilalabwe na Logombo kuilalamikia Tanesco na kuiomba Serikali kuingilia kati.
Mkazi wa Ilalabwe, Isaya Mwansusyo alisema baada ya kuona wenzao jirani wamefungiwa umeme, walifuatilia kwa watu walioamini ni wafanyakazi wa Tanesco kwa kuwa walikuwa wanatumia magari yenye nembo ya shirika hilo.
Hata hivyo, Bahati alikanusha tuhuma hizo, akisema katika kipindi cha mradi huo, magari ya Tanesco yalikuwa mabovu.
Mwansusyo alisema, wakiamini watu hao ni watumishi wa Tanesco, waliwaambia wachange fedha kwa ajili ya kununua nguzo, nyaya na mita na wao walifanya hivyo na kupelekewa vifaa hadi kufungiwa umeme.
Alisema walichanga Sh200,000 kwa ajili ya nguzo na Sh102,000 kwa ajili ya mita na nyaya kila mmoja huku baadhi wakitoa kiasi kikubwa zaidi ya hicho.
Mwenyekiti wa Ilalabwe, Daud Kajemba alisema suala hilo linawahusisha Tanesco moja kwa moja, hivyo aliiomba Serikali kuingilia kati na kufanya uchunguzi wa kina.
Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Chalya Julius alisema awali, alipokea malalamiko ya wananchi kwamba watu wa Tanesco wanafanya ujanja wa kuhamisha nguzo na kuzipeleka maeneo mengine.
“Nilichokifanya ni kuwaita Tanesco kujibu malalamiko hayo, lakini walichosema ni kuwa wao ni wasimamizi tu wa kampuni zinazosambaza umeme wa Rea, hivyo nikaagiza nguzo hizo zitafutwe popote na wahusika wakamatwe,” alisema.
Alisema kwa kuwa kila kampuni ina namba zake za siri kwenye nguzo, walipokwenda kwenye vijiji ambavyo awamu ya pili ya usambazaji umeme ilikuwa imesimama walizikuta na wananchi wakiwa tayari wamefungiwa umeme na unawaka.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohammed Mpinga alisema katika tukio hilo waliwakamata watu 22 na 17 kati yao ni wananchi waliokuwa wamefungiwa umeme na wengine ni waliojihusisha kuchangisha fedha.
Alisema waliamua kuwaachia kwa dhamana kwa kuwa uchunguzi wa shauri hilo utachukua muda mrefu.
Watu wanne tunawafuatilia kwa ukaribu katika tukio hili, wakiwamo wahandisi na watunza stoo wa vifaa. Tunaamini upelelezi huu utachukua muda mrefu kutokana na kukosa ushirikiano wa dhati kutoka kwa watu wa Tanesco,” alisema.

No comments:
Post a Comment