Sunday, October 15

UNDP kutokomeza umaskini ifikapo 2030


Moshi. Shirika la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa kushirikiana na Tanzania wameungana kutokomeza umaskini duniani ifikapo mwaka 2030.
Mkuu wa mawasiliano wa Umoja wa Mataifa, Hoyce Temu alisema Tanzania ni moja ya nchi iliyoridhia kutokomeza umaskini.
“Kama tunavyoelewa kuwa Tanzania vijana wanafikia zaidi ya asilimia 65 na malengo haya ni ya miaka 15 kwa hiyo walengwa wakubwa wa malengo hayo ni vijana,” alisema Temu.
Alifafanua kuwa ili kuhakikisha malengo hayo yanawafikia vijana wengi, wamewahamasisha wanafunzi wa Shule ya Sekondari Weruweru iliyopo wilayani Moshi ikiwa ni muendelezo wa mipango yao ya kuwafikia vijana katika vyuo, shule za sekondari na za msingi ili kutoa elimu ya malengo ya dunia.
Mwakilishi mkazi wa UNDP, Alvaro Rodriguez alisema wametoa kipaumbele kwa wanafunzi wa kike katika Shule ya Weruweru kwa nia ya kuhitaji viongozi wengi wanawake nchini.

No comments:

Post a Comment