Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema si jambo linalikubalika na kwamba inashangaza kuona zaidi ya watoto 8,000 wameuwawa na kujeruhiwa katika migogoro kwa kipindi cha mwaka uliopita.
Katika ripoti hiyo ambayo Shirika la habari la AP ilipata nakala yake, katibu mkuu amevitaka vikosi vya ulinzi kuongeza jitihada zaidi katika kuwalinda wasichana na wavulanakatika matiafa ya Yemen, Syria, Congo na Afghanistan. Ripoti imehakiki maovu dhidi ya watoto 3,512 nchini Afghanistan ikiwa ni zaidi ya asilimia 40 ya idadi jumla ya matendo hayo. Kiwango hicho kinatajwa pia kuwa ni kikubwa kuwahi kufikiwa nchini humo.
Aidha Guterres amesema kiwango cha kuwaandikisha na kuwatumikisha watoto katika maeneo yenye vita kimeongezeka mara dufu katika matiafa ya Somalia na Syria ikilinganishwa na mwaka wa 2015. Umoja wa Mataifa umethibitisha matukio 169 ambayo yamewaathiri watoto 1,022 huko Sudan ya Kusini ambpo asilimia 60 miongoni mwao wameingizwa katika upiganaji na wanatumiwa na vikosi vya serikali.
Unyanyasaji wa kingono waongezeka maradufu
Vilevile idadi ya visa vya unyanyasaji dhidi ya watoto vinavyofanywa na makundi ya wenye itikadi kali kama al Shabaab, Boko Haram, Kundi la Dola la Kiislamu na Taliban vinafikia 6,800. Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric amesema katika taarifa ya Guterres Msemaji wa U.N. Stephane Dujarric alisema katika taarifa kwamba Guterres"ameshangwa" si tu kwa watoto zaidi ya 8,000 waliouawa na kujeruhiwa na kusajiriwa jeshini lakini pia kwa unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wasichana na wavulana na mashambulizi yanayofanyika katika maeneo ya shule na hospitali.
Virginia Ganmba, ambae ni mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya watoto na migogoro inayohusisha silaha amesema "Mtoto anauwawa, anasajiriwa jeshini, anajeruhiwa katika shambulio au kuzuiliwa asiendelee na masomo yamekuwa mengi yanaxyomzonga."
Ripoti hii mpya ya Umoja wa Mataifa kuhusu madhira ya watoto katika maeneo ya vita imeorodhesha vikosi vya serikali, makundi ya waasi ambayo yanasajiri watoto, kuwatumia, kuwauwa, kuwajeruhi, kuwabaka, kuwatumikisha kingono, kuwateka watoto au kushambulia shule na hospitali. Kwa mara ya kwanza kabisa kwa mwaka huu Guterres ameigawanya orodha hiyo katika sehemu mbili. Moja inataja vyama ambavyo havichukui hatua zozote kuboresha namna ya kuwalinda watoto na nyingine ambayo inahusisha makundi yaliyochukua hatua.
No comments:
Post a Comment