“Ujumbe wangu ni kwamba Kenya inaimarika kidemokrasia. Kenya imethibitisha kuwa inaweza kwenda kwenye uchaguzi wa urais, ukafutwa na ikakubalika na kisha Wakenya wakapata nafasi ya kurudi,” amesema Rais Uhuru leo Alhamisi Oktoba 26,2017 alipojibu maswali ya waandishi wa habari baada ya kupiga kura.
“Tunatakiwa wote twende mbele. Sisi Wakenya tunakwenda mbele baada ya Wakenya kutumia haki yao kidemokrasia,” amesema.
Amewataka Wakenya kutowabughudhi maofisa wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), kwa sababu wameruhusiwa kusimamia uchaguzi ambao kila Mkenya ana haki ya kushiriki.
Rais Uhuru amepiga kura katika kaunti ya Kiambu eneo la Gatundu akisindikizwa na mkewe, Margaret Gakuo.
No comments:
Post a Comment