Taarifa ya DSE inazitaja kampuni ambazo hisa zake zimeongoza kushuka kuwa ni Uchumi Supermarket (USL) kwa asilimia 22, Shirika la Ndege la Kenya (KA) asilimia 16 na Acacia kwa asilimia tisa.
Mauzo ya soko hilo kwa kipindi cha wiki moja yameshuka kutoka Sh53 bilioni mpaka Sh3 bilioni baada ya hisa 800,000 za kampuni za ndani kuuzwa kati ya Septemba 25 hadi Septemba 29.
Wiki iliyoishia Septemba 22, jumla ya mauzo ilikuwa Sh53 bilioni, lakini wiki iliyoishia Septemba 29 yalikuwa Sh3 bilioni.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, USL ilianza wiki ikiuza hisa kwa Sh90 lakini ikamaliza kwa Sh70 wakati KA ilianza na Sh120 na ikahitimisha kwa Sh100. Hisa za Acacia ambayo inaendelea na mazungumzo na Serikali baada ya kuzuiwa kusafirisha mchanga wa madini zilikuwa zinauzwa Sh5,480 mwanzo mwa wiki hiyo lakini zilishuka mpaka Sh4,980.
Bei ya hisa za Acacia zimepungua kutoka Sh12,500 kabla ya zuio hilo, Machi mwaka huu. Wakati suala la mchanga likiitesa Acacia, maduka ya Uchumi yanakabiliwa na madeni ya bidhaa inazoletewa kiasi cha Serikali ya Kenya inakotoka kuahidi kuisaidia kuyalipa.
Ofisa Masoko Mwandamizi wa DSE, Mary Kinabo alisema kupungua kwa hisa zilizouzwa kutoka milioni nne hadi 800,000 kumechangia kuporomoka kwa mapato hayo.
Hata ukubwa wa mtaji wa kampuni zilizoorodheshwa sokoni hapo umepungua kwa Sh115 bilioni. “Wiki iliyoishia Septemba 23 ulikuwa Sh20.5 trilioni lakini Septemba 29 ulikuwa Sh20.3 trilioni,” alisema Kinabo.
Hata hivyo, ukubwa wa mtaji wa kampuni za ndani umeongezeka kwa Sh71 milioni kutoka Sh9.6 trilioni hadi Sh9.7 trilioni kutokana na kupanda kwa bei ya hisa za Kampuni ya Sigara (TCC) iliongoza kwa kwa asilimia 66 ikifuatiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa asilimia 27 na Benki ya CRDB asilimia mbili.
No comments:
Post a Comment