Hata hivyo, ingawa Rais Uhuru Kenyatta amesisitiza yuko tayari kwa uchaguzi huo na utaendelea, mgombea wa upinzani Raila Odinga alijiondoa wiki iliyopita.
Jana, Bw Odinga, ambaye ni mgombea wa muungano wa National Super Alliance (Nasa) alitangaza kwamba siku hiyo badala ya kushiriki uchaguzi, wafuasi wake watafanya maandamano makubwa kote nchini.
Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati siku ya Jumatano alikuwa amewalaumu wanasiasa wa kusababisha kuwepo kwa mazingira yanayoifanya vigumu kuandaa uchaguzi huru na wa haki.
Alisema alikuwa anawapa "kadi ya manjano".
Waziri wa usalama wa ndani Dkt Fred Matiang'i tayari ametangaza Alhamisi kuwa siku ya mapumziko.
No comments:
Post a Comment