Monday, October 2

Trump: Mazungumzo na Korea Kaskazini ni kupoteza muda

A combination photo of Donald Trump and Kim Jong-unHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionTrump: Mazungumzo na Korea Kaskazini ni kutupa muda
Rais wa Marekani Donald Trump amemwambia waziri wake wa mashauri ya nchi za nje kuwa anapoteza muda wake akijaribu kufanya mazungumzo na Korea Kaskazini kuhusu mpango wake wa nyuklia.
"Jiwekee nguvu zako Rex, tutafanya kile kitahitajika kufanywa," Bw. Trump aliandika kwenye twitter baada ya kuibuka madai kuwa Marekani ilikuwa kwenye mazungumzo na Pyongyang.
Rex alifichua hayo siku ya Jumamosi akisema kuwa Korea Kaskazini haitili maanani mazungumzo hayo.
Nchi hizo mbili zimekuwa kwenye majibizano makali miezi ya hivi karibuni.
Marekani inataka Korea Kaskazini kusitisha mipango yake ya silaha baada ya kufanya majaribio kadha ya makombora ya na kudai kufanya jaribo la bomu la haidrojeni ambalo linaweza kutundikwa kwa kombora la masafa marefu.
Hi sio mara ya kwanza Donald Trump amekinzana na maafisa wa vyeo vya juu kwenye utawala wake.
Mwezi Agosti alisema kuwa jeshi la Marenia lilikuwa tayari kukabiliana na Korea Kaskazini, saa chache baada ya waziri wake wa ulinzi kujaribu kutuliza misukosuko akisema kuwa jitihada za mazungumzo zilikuwa zinafanikiwa.
Matamshi yake yanakuja siku moja bada ya Bw Tillerson kufichua kuwa maafisa wa Marekani walikuwa na mawasiliano na Korea Kaskazini licha na kuwepo vita vya maneno kati ya viongozi wa nchi hizo mbili.

No comments:

Post a Comment