Monday, October 2

Kifo cha Kim Jong-nam: Wanawake wakana mashtaka nchini Malaysia

Vietnamese Doan Thi Huong (L) and Indonesian Siti Aishah are seen in this combination picture from undated handouts released by the Royal Malaysia Police to Reuters on 19 February 2017Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionKifo cha Kim Jong-nam: Wanawake wakana mashtaka nchini Malaysia
Wanawake wawili wamekana mashtaka ya kumuua Kim Jong-nam, ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini, wakati wa kuanza kwa kesi yao nchini Malaysia.
Bwana Kim alifariki mwezi Februari kwenye uwanja wa Kuala Lumpur, katika kisa cha kusikitisha kilicho ishangaza dunia.
Mwaname raia wa Vienam Doan Thi Huong, 29 na mwingine raia wa Indonesia Siti Aisyah, 25, wanalaumiwa kwa kumwekea kemikali hatari ya VX usoni, alipokuwa akisubiri kuabiri ndege kwenye uwanja wa Kuala Lumpur.
Lakini wanawak hao wamedai kuwa maajenti wa Korea Kaskazini waliwahadaa kufanya hivyo.
Kim Jong-nam at the Beijing International airport, 25 September 2004Haki miliki ya pichaAFP
Image captionBw Kim alisafiri mara kwa mara barani Asia na alionekana mjini Beijing mwaka 2004
Pyongyang imekana kuhusika kwa vyovyote vile kwenye mauaji hayo
Wanawake hao walikuwa wamefungwa mikono na kuvaa mavazi yasiyopenya risasi, kwa mujibu wa shirika la AFP
Ikiwa watapatikana na hatia wanawake hao watahukumiwa kifo. Mawakili wao wanasema kuwa washukiwa wakuu wameondoka nchini Malaysia.
Kisa hicho kilisababisha mzozo wa kidiplomasia na kuharibika kwa uhusiano kati ya Korea Kaskazini na Malaysia ambapo kila nchi iliwatimua mabalozi wa nchi nyingine.

No comments:

Post a Comment