Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeadhimisha siku ya Viwango Dunia kwa kutoa zawadi na vyeti kwa wanafunzi walioshinda shindano la uandishi wa Insha kama sehemu sehemu ya maadhimisho hayo na pia kuwajengea uwezo na uelewa wanafunzi juu ya umuhimu wa viwango. Mkurugenzi Mkuu wa TBS, Prof.Egid Mubofu alisema shirika lake linaipa siku ya viwango duniani kwa kuwajengea uwezo vijana kwa kuwashindanisha kwenye uandishi wa insha.
“Lengo kubwa la maadhimisho haya ni kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa viwango katika kuboresha maisha ya wananchi katika ubora wa vitu vyao, afya , usalama na biashara,” alisema Prof.Mubofu Prof. Mubofu alisema kila mwaka Shirika la Viwango Duniani huwa na Kauli mbinu yake ambayo kwa mwaka huu ni “Viwango huifanya Miji kuwa ya Kisasa zaidi” ambapo kauli mbiu hii inaweka msisitizo kupitia viwango uboreshaji wa maisha ya wakazi wa mijini kuwa ya kisasa zaidi.
“Shirika huandaa mashindano ya Insha katika shule za sekondari kupitia kauli mbinu ya mwaka ya viwango lengo ikiwa kupima uwezo wa wananfunzi katika ufahamu wao kuhusu viwango,” alisema Prof.Mubofu Alisema hii inatoa nafasi ya kupima kwa namna gani wananchi wanaelewa juu ya umuhimu wa viwango na kipi kifanyike katika kuwajengea uwezo hasa wanafunzi katika kuelewa juu ya majukumu na umuhimu wa viwango katika maisha yao.
Prof.Mubofu alisema TBS imetoa zawadi pamoja na vyeti kwa washindi wa insha ikiwa ni motisha ilikuchochea ushiriki wa wanafunzi wengine katika mashindano mbalimbali yanayotolewa na shirika kuhusu umuhimu wa viwanda. Aliongeza kuwa kutoka na ushiriki wa wanafunzi katika shindano hilo kuwa mkjubwa, TBS imejipanga kuboresha vigezo vya ushiriki ili kutoa nafasi kwa wanafunzi wa ngazi zote kushiriki kikamilifu.
“ TBS imejipanga kuboresha maisha ya watanzania kwa kusimamia viwango vya ubora katika maeneo yote hasa uzalishaji na ujenzi na afya,” alisema Prof.Mubofu na kuongeza kuwa azma ya serikali ya awamu ya tano ya kuwa nchi ya uchumi wa kati na viwanda itatekelezeka kwa kuwa na usimamizi madhubuti wa viwango.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa uandaaji viwango TBS, Bi. Edna Ndumbaro alisema matumaini ya TBS kupitia mashindano ya insha katika maadhimisho ya siku ya viwango duniani ni kuwapatia uelewa na elimu kuhusu maswala ya viwango kwa manufaa ya sasa na jamii ijayo.
“Wanafunzi 10 kutoka Shule za sekondari za Kibaha,Feza, Elboru na Loyola walipatiwa zawadi ikiwa ni ishara ya kuifanya elimu ya viwango kuwa endelevu,” alisema Bi.Ndumbaro Mshindi wa kwanza wa shindano la Insha alikuwa mwanafunzi kutoka shule ya Sekondari Kibaha,Bw. Barnabas Michael ambaye alisema kushiriki kwenye mashindano kunamfanya mwanafunzi kujijengea uwezo wa kujieleza na pia kuwa na ufahamu wa mambo kwa mapana yake.
“Wito wangu kwa wanafunzi wenzangu ni kujitokeza kwa wingi kushiriki katika mashindano mbalimbali kwani yanasaidia kuongeza maarifa na uwezo wa kupambanua mambo mbalimbali,” alisema Bwana Michael Siku ya Viwango Duniani uazimishwa kwa lengo la kuelimisha juu ya uelewa miongoni mwa mamlaka za udhibiti, viwanda na walaji kuhusiana na umuhimu wa viwango kwa uchumi wa dunia ikiwepo Tanzania.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania(TBS) Prof.Egid Mubofu akitoa mada kwenye hafla ya maadhimisho ya Siku ya Viwango Duniani yaliyofanyika katika ofisi za shirika hilo Ubungo jijini Dar salaam. Katika maadhimisho hayo yaliambatana na utoa wa vyeti na zawadi kwa wanafunzi walioshinda katika shindano la uandishi wa insha uliendana na kauli mbiu ya maadhimisho ambayo ni “VIWANGO HUIFANYA MIJI KUWA YA KISASA ZAIDI”
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania(TBS) Prof.Egid Mubofu akikabidhi zawadi ya Laptop, cheti na Kiasi cha shilingi laki tatu na nusu kwa mshindi wa Kwanza wa uandishi wa Insha mwanafunzi Shule ya Sekondari Kibaha Bw. Barnabas Michael katika shindano maalum la kuadhimisha siku ya viwango Duniani ikiwa na kauli mbiu “VIWANGO HUIFANYA MIJI KUWA YA KISASA ZAIDI” . shindano hilo limelenga wanafunzi kwa lengo la kuandaa kizazi chenye uwelewa wa kutosha juu ya umuhimu wa viwango katika ubora, Afya, Usalama na Biashara.
No comments:
Post a Comment