Thursday, October 12

SERIKALI: RASILIMALI ZA BAHARI ZITUMIKE KWA MASILAHI YA WATANZANIA

Serikali  imesema kuwa itahakikisha rasilimali za bahari zinatumika kwa ajili ya watanzania Wote

Hayo aliyasema Waziri, Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar, Ahmad Rashid alipofanya ziara ya ukaguzi wa  meli ya  uvuvi  katika bandari ya Zanzibar mapema leo.

Rashid amesema  kuwa rasilimali za baharini zikitumika  ipasavyo zinaweza kuleta maendeleo na kuhakikisha uvuvi unaofanyika katika bahari unafuata taratibu  kwa masilahi ya taifa .

Katika ukaguzi  huo wa meli hiyo Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar, Ahmad Rashid pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo na Mifugo, Abdallah Ulega wametembelea ofisi za utoaji leseni wa meli za uvuvi  ya  serikali ya mapinduzi Zanzibar .

Amesema sheria iko wazi  kwa hivyo  lazima rasilimali za Tanzania  ikiwemo na bahari iwanufaishe watanzania  wote bila kujali vyama vyao.

Nae Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvia, Abdallah Ulega amesema  serikali zote mbili zitahakikisha rasilimali za bahari  zinatumiwa na watanzania na sio kwa wageni tu. Amesema watasimamia sheria za uvuvi katika kulinda rasilimali za bahari ili ziweze kuleta maendeleo kwa watanzania.

Nae Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Zanzibar, Hosea Mbilinyi  amesema  mamlaka imepiga hatua katika  kuhakisha rasilimali za bahari zinanufaisha Tanzania
 Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Zanzabar, Ahmad Rashid akizungumza katika ukaguzi wa Meli ya Uvuvi ya China katika bandari ya Zanzibar.
 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega akizungumza baada ya ukaguzi wa meli ya uvuvi wa China katika Bandari ya Zanzibar ili kujionea shughuli za uvuvi katika eneo hilo.
 Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Zanzabar, Ahmad Rashid(kulia) na  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega(kushoto) wakiwa wameshika Samaki ambaye amevuliwa na Meli ya Uvuvi yaa China katika Bandari za Zanzibar .
 Wavuvi wakiendelea na kazi.
Muonekano wa Meli ya Uvuvi ya China katika bandari ya Zanzibar. Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii.

No comments:

Post a Comment