Mapacha waliokuwa wamezaliwa wakiwa wameshikana katika kijiji cha mbali nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo, wameponea safari ya saa 15 kwa njia ya piki piki wakipelekekwa kutenganishwa.
Kisha wakasafirishwa kwa njia ya ndege hadi mji mkuu Kinshasa, ambapo walifanyiwa upasuaji na kundi la madaktari wa kujitolea
Kwa jumla watoto hao wa wiki moja, walifanya safari ya kilomita 1,400 ya barabara mbovu na kwa njia ya ndege.
Watoto hao Anick na Destin, watarudishwa kijijini wao baada ya majuma matatu. Walizaliwa baada ya uja uzito wa wiki 37 mwezi Agosti.
Karibu mmoja kati ya watoto 200,000 huzaliwa wakiwa wameshikana, na kuishi kwao huwa finye hasa sehemu za mbali ambapo hakuna huduma za kiafya.
Lakini mapacha hawa walizaliwa kawaida tu katika kijiji cha Muzombo magharibi mwa DRC.
Walipogundua kuwa watoto hao walihitaji kufanyiwa upasuaji wazazi wao Claudine Mukhena na Zaiko Munzadi, waliwafunga blanketi na kuanza safari kupitia msituni kwenda hospitali iliyokuwa karibu.
Kutokana na ukosefu wa vifaa na ujuzi wa kufanya upasuaji huo katika hospitali ndogo, madakaktari waliwahamisha kwenda mjini Kinshasa karibu umbali wa maili 480.
Kufika mjini Kinshasa familia hiyo ilisafirishwaa na ndege ya shirika la MAF, la kutoa huduma za kibinadamu.
"Wako salama, wanalala vizuri na kula vizuri kwa jumla, wako salama," Dr Junior Mudji alisema.
"Watakuwa hapa kwa wiki tatu zaidi kuhakikisha kuwa kila kitu kiko sawa,"
Dr Mudji anaamini upasuaji huo nduo wa kwanza wa kuwatenganisha mapacha walioshikana nchini Jamhuri ya Demokrasi ya Congo.
No comments:
Post a Comment