Monday, October 23

Rais wa Botswana ashiriki kuokoa raia wake


Gaborone, Botswana. Rais wa Botswana, Luteni Jenerali Seretse Khama Ian Khama juzi ameonyesha mapenzi makubwa kwa raia wake baada ya kushiriki oparesheni ya kumsaka na kumuokoa rai wake mmoja aliyepotea msituni wakati akitafuta ng’ombe wake.
Shirika la habari la serikali limeripoti kwamba Khama alikwenda hadi kijijini kwake katika mji wa Mosu, kabla ya kuruka kwa helikopta kuungana na watu wengine katika shughuli ya kumsaka mtu huyo.
Khama na timu yake aliruka na helikopta hiyo katika maeneo matatu tofauti huku timu nyingine ikiwa ardhini na hatimaye walitambua mahali alipokuwa mtu huyo isipokuwa changamoto kubwa ilikuwa mawasiliano na namna ya kufika.
“Hatimaye timu zote mbili za uokoaji yaani ya angani na ardhini zilitambua mahali alipo mtu huyo. Helikopta iliyokuwa na watu saba ikiendeshwa na rais ilikuwa na marubani wengine wawili na wafanyakazi watano ilitua msituni na baadaye ikamchukua mtu huyo ikamsafirisha hadi kliniki ya Mokubilo.
“Baada ya mtu huyo kupatikana, alikuwa mchovu aliyeonekana kutokuwa na maji mwilini na hakuwa na uwezo wa kutembea. Timu ya uokoaji ilimpatia maji na juisi kumwongezea sukari mwilini ili kumwezesha kupata nguvu kabla ya kumpeleka hospitalini.”
“Mara baada ya kufika Mokubilo, alisafirishwa hadi Hospitali ya Letlhakane kwa ajili ya kupatiwa matibabu stahiki na kupata uponyaji na akalazwa.
“Inafaa ieleweke kwamba eneo hilo kuna wanyama pori hasa wanyama wakali kama chui na simba na tembo,” ilisema taarifa ya serikali kuhusu tuhio hilo lililotokea Oktoba 21.

No comments:

Post a Comment