Monday, October 16

‘Rais asingetangaza nyongeza hadharani’


Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta) mbali na kupongeza uamuzi wa Serikali kuboresha mishahara ya watumishi wa umma, limesema lingeshirikishwa lingeshauri nyongeza hiyo isitangazwe hadharani.
Katibu Mkuu wa Tucta, Dk Yahya Msigwa alisema madhara ya kutangaza hadharani nyongeza hiyo ni kwa wafanyabiashara kupandisha bei ya bidhaa na huduma.
“Kama Tucta tungeshirikishwa tungeshauri marekebisho ya nyongeza za mishahara isitangazwe hadharani kwa kuwa itasababisha gharama kupanda,” alisema.
Juzi, akiwa Zanzibar kwenye kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru, Rais John Magufuli alitangaza kuwa watumishi wa umma watarekebishiwa nyongeza za mishahara yao.
Alisema kwa kuanzia, watumishi wa umma 59,027 wanarekebishiwa mishahara yao inayogharimu Sh103 bilioni. Magufuli alisema Serikali itakuwa ikifanya marekebisho ya mishahara ya watumishi wa umma kila itakapokuwa inapata uwezo.

No comments:

Post a Comment