Wakati wanafunzi wa darasa la nane wakitarajia kuanza mitihani ya kuhitimu kuanzia kesho, kiongozi wa muungano wa upinzani wa Nasa, Raila Odinga ameendelea kumshambulia Rais Uhuru Kenyatta akimtaka kuachia madaraka.
Wanafunzi nchini humu wanatarajia kuanza mitihani hiyo huku hali ya usalama ikiwa bado tete kufuatia uchaguzi wa urais wa marudio uliofanyika wiki iliyopita.
Akizungumza kwenye ibada ya Jumapili iliyofanyika katika kanisa la Gatina PAG, Odinga alisema mauaji ya watu watatu juzi katika eneo la Kawangware mjini Nairobi hayakubaliki. Watu watatu waliuawa na wanaodaiwa kuwa ni polisi baada ya kutokea sintofahamu kati ya polisi na waandamanaji.
Mwanasiasa huyo aliyesusia uchaguzi wa marudio alisema kwamba siasa za Kenya zimehamia katika uhasama wa kushambuliana baina ya raia na vyombo vya usalama.
Siku ya Ijumaa, watu watatu waliuawa na wengine kujeruhiwa baada ya makundi mawili pinzani kupigana mgogoro unaohusishwa na kuibuka kwa kundi la Mungiki.
Hata hivyo, Odinga alisema katika hotuba yake kanisani jana kuwa, umaarufu wake ni wa nchi nzima na kwamba Rais Kenyatta anatumia ‘nguvu ya kutawala’.
“Wakenya wanataka haki si utawala wa nguvu. Tuko katika barabara ya Kanaani na safari bado inaendelea. Kenya inahitaji kiongozi asiye na ubinafsi ili kukabiliana na ubaguzi ambao Jubilee haiwezi kuutatua,” alisema,
Watu 49 wanadaiwa kuuawa na vyombo vya dola nchini humo vifo vinavyohusishwa na uchaguzi huo ambapo vimetokea kati ya Agosti 8 na juzi wengi wakiuawa katika maeneo ya Kawangware, Kibera, Mathare na Kisumu.
Vifo vilivyotokea Kawangware juzi vimeelezwa kutokea kutokana na ‘vita’ ya kawaida kati ya polisi na waandamanaji vilivyosababisha kuibuka kwa makundi mawili yenye mrengo wa kikabila.
Pande zote zilikuwa na silaha kama mapanga, visu, marungu na mawe, ambapo polisi walisema walimuua mtu mmoja, lakini wananchi wanadai watu wengi walikufa au kupotea kutokana na mapigano.
Nini kilichosababisha?
Kila upande unaulaumu mwingine, lakini ukabila ndio unaoelezwa kusababisha mapigano hayo ikielezwa kwamba yaliongozwa na ufuasi wa kisiasa ulioegemea katika mrengo huo.
“Tulidhamiriwa kwa sababu hili ni eneo la Wakikuyu,” anasema Geoffrey Mbithi (42) anayejishughulisha na shughuli za hoteli ambaye nyumba yake ya wageni iliharibiwa.
Machafuko hayo ingawa yalikuwa ya kipekee na yaliyodumu kwa saa chache yalikumbushia ukatili wa kikabila uliosababishwa na siasa ambao huchochea vurugu zilizosababisha vifo vya watu zaidi ya 1,100 miaka 10 iliyopita.
“Mimi nilikuwa ndani ya nyumba nikasikia watu wakisema, ‘moto, moto, moto,” alisema Rose Kiema mwenye umri wa miaka 50 ambaye ameishi na kufanya kazi katika eneo la Congo Junction tangu miaka ya 1980.
Mama huyo alikimbia na kurejea kesho yake asubuhi na kukuta moshi ukiendelea kufuka katika makazi yake.
Karibu na sehemu hiyo kuku watatu na mbuzi walichomwa moto wakiwa hai.
Kiema na wenzake wanasema vijana ambao ni wafuasi wa Nasa walichoma moto huo wakichagiza lengo la viongozi wao la kutoshiriki uchaguzi.
“Tulifanyiwa unyama huu kwa sababu hatuiunga mkono Nasa. Tulipiga kura, ndiyo sababu pekee tunayopata tabu,” anasema Josphat Gatimu (62).
Hakukuwa na huruma kwa wachuuzi wa bidhaa mbalimbali raia kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambao walishuhudia bidhaa zao zikichomwa moto.
“Mahali hapa ni ngome ya Nasa,’’ alisema mtu mmoja mwenye umri wa miaka 20 ambaye hakutaka kutaja jina lake.
“Ni nini kinachoendelea hapa? Ni Serikali inajaribu kulazimisha vikundi vingine vibaya kutoka katika jumuiya zingine kuja na kutishia usalama wetu,” alisema akimaanisha ‘Mungiki’, kikundi kinachohusishwa na Wakikuyu kinachojulikana kwa harakati za kikabila.
Wakati wa uchaguzi wa mwaka 2007, Rais Kenyatta alishutumiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai kuchochea vurugu za kisiasa jambo ambalo alitumia muda mwingi kulikanu
No comments:
Post a Comment