Tuesday, October 17

NASSARI AWASILISHA USHAHIDI WA TATU TAKUKURU


Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari(kulia), akiongazana na Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea(katikati), kuingia ofisi za Takukuru, Dar es Salaam jana kupeleka awamu ya pili ya ushahidi wa tuhuma za madiwani kununuliwa. Kulia ni Mwenyekiti wa Chadema jimbo la Arumeru Mashariki, Gadiel Mwanda. Picha na Loveness Bernard

MBUNGE wa Arumeru Mashariki,  Joshua Nassari (Chadema), amewasilisha ushahidi wa tatu wa picha za video juu ya tuhuma za kununuliwa madiwani wa Chadema na viongozi wa Serikali mkoani Arusha kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru).
Ushahidi huo   ni wa tatu baada ya kuwatuhumu Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Mnyeti na Mkurugenzi wa wilaya hiyo, kuwanunua madiwani hao   wajiunge na CCM
Nasari alifika Takukuru saa 8.300 mchana akiwa ameongozana na Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea.
Madiwani hao wanane wa Chadema walijiuzulu kwa kile walichoeleza kumuunga mkono Rais John Magufuli jambo ambalo Nassari anadai siyo kweli bali walinunuliwa.
Akizungumza na waandishi wa habari   Dar es Salaama jana nje ya ofisi ya Takukuru Upanga, alisema huo ni ushahidi wa tatu na kadri upepelezi unavyoendelea atawasilisha ushahidi mwingine kwa sababu  suala hilo ni kama   ‘filamu ya Isidingo’.
Alisema alitarajia Rais Dk. John Magufuli angewachukulia hatua wateule wake wanaohusishwa katika suala  hilo   kupisha uchunguzi uweze kufanyika kwa uhuru.
“Tunajiuliza kwa nini Rais hawachukulii hatua DED, DAS au DC wote wa Arumeru kwa kutuhumiwa… tungeomba suala hili lichukuliwe kwa uzito wake,” alisema
Alisema alifarijika kuona mmoja wa madiwani anayetuhumiwa kupokea rushwa ameitwa kuhojiwa na Takukuru wilayani Arumeru.
Alisema alisikitishwa na taarifa zilizoandikwa na chombo kimoja cha habari kikiwanukuu Takukuru wakidai kuwa uchunguzi utachukua muda mrefu kutokana na kuwa gumu jambo ambalo lilimkatisha tama.
“Naamini hatua zitaenda kuchukuliwa kwa kuwa mpaka leo hii hakuna hata mmoja aliyekanusha wala kukubali,” alisema Nassari.
Alisema amepeleka ushahidi wa picha za video na pia anao mashahidi wa baadhi ya madiwani waliokuwa wakifuatiliwa na viongozi hao na wakakataa.

No comments:

Post a Comment