Tuesday, October 31

Mtu aliyepanga kumuua Rais Vladimir Putin ajeruhiwa Ukrain

Volunteer fighter Amina Okuyeva cleans her assault rifle. Photo: July 2014Haki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionAmina Okuyeva na mumewe walipigana dhidi ya makundi yanayoiunga mkono Urusi
Mwamamue moja kutoka Chechenia ambaye analaumiwa kwa kupanga kumuua rais wa Urusi Vladimir Putin amejeruhiwa na mke wake kuuliwa wakati wa shambulizi karibu na mji mkuu wa Ukrain Kiev.
Adam Osmayev alijeruhiwa lakini anaweza kuishi baada ya gari alilokuwa akilitumia kumiminiwa risasi kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani ya ukrain.
Wizara hiyo ilisema kuwa mke wake Osmaye, Amina Okuyev aliuawa wakati wa shambulizi katika kijiji cha Hlevaha.
Mwaka 2012 maafisa nchini Urusi walisema kuwa Bw. Osmayev alikuwa sehemu ya njama ya wanamgambo kumuua Bwa Putin.
Vyombo vya habari vya Urusi viliripoti wakati huo kuwa watu walipanga kutega mabamu kwenye barabara ya Kutuzovsky mjini Moscow, inayotumiwa na Bw Putin kila siku.
map
Image captionUkrain
Urusi baadaye iliitaka Ukrain kumsalimisha Bw. Osmayev lakini mamlaka nchini Urusi zikakataa kufanya hivyo, zikisema kuwa zilitaka kungoja hadi mahakama ya haki za binadamu ya Ulaya kuamua kuhusu ombi lake la kupinga kusalimishwa kwa Urusi.
Mwezi Juni alinusurika jaribio la kumuua mjini Kiev. Mshambuliaji kisha akapigwa risasi na kujeruhiwa na Bi Okuyeva.
Hakuna mtu aliyedai kuhusika kwenye shambulizi la siku ya Jumatatu.
Hii inakuja chini ya wiki moja baada ya mbunge wa Ukrain kujeruhiwa kwenye shambulizi la bomu kwenye mji mkuu Kiev.
Mlinzi wa Ihor Mosiychuk na mtu mwingine waliuawa wakati wa mlipuko huo.
Bi Okuyeva wakati moja alifanya kazi kama mshauri wake.

No comments:

Post a Comment