Tuesday, October 31

Mabadiliko ya hali ya hewa yanaathiri afya

Athari za mabadiliko ya hali ya hewa
Image captionAthari za mabadiliko ya hali ya hewa
Ripoti mpya ya mabadiliko ya hali ya hewa imeonyesha kuwa kuongezeka kwa joto kunaathiri afya ya binaadam kwa kiasi kikubwa.
Ripoti hizo kutoka kundi la vyuo mbalimbali na mashirika tofauti ya umoja wa mataifa zinasema watu wengi wanaathirika na joto pamoja na mlo hafifu sambamba na kusambaa kwa magonjwa.
Viwanda vinatajwa kwa kiwango kikubwa kuchangia mabadiliko ya hali ya hewa
Image captionViwanda vinatajwa kwa kiwango kikubwa kuchangia mabadiliko ya hali ya hewa
Katika toleo la Lancet wamesema njaa kwa kiasi kikubwa zinasababishwa na ongezeko la joto linalopelekea mimea kukauka.
Wameonyesha pia uwezekano wa kusambaa zaidi kwa ugonjwa wa malaria kutokana na mazingira kutokuwa safi.

No comments:

Post a Comment