Mbowe amewaambia wanahabari kwamba kwa mujibu wa madaktari, hali ya Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu imeimarika hivyo wakati wowote kuanzia wiki ijayo anaweza kutolewa hospitali.
"Bw Lissu ametolewa katika chumba cha wagonjwa mahututi na kuwekwa katika wodi ya kawaida huku akiwa na uwezo kamili wa kuongea na kutembea kwa kutumia kiti cha magurudumu," alifafanua Mbowe. Hata hivyo, Chadema imesema kuwa, kwa kuhofia usalama wa Lissu, kwa sasa hawatamrudisha nchini Tanzania.
"'Kwa sababu za kiusalama hatutaweza kusema atakwenda wapi lakini itoshe tu kuwaambia kuwa ataanza awamu ya tatu ya matibabu nchi nyingine, sio Tanzania wala sio jirani''
- Familia ya Tundu Lissu yataka wapelelezi wa kimataifa kuingilia kati
- Mbowe: Madaktari wana matumaini kuhusu Tundu Lissu
Tundu Lissu alipigwa risasi zaidi ya thelathini na watu ambao mpaka sasa hawafahamiki mwanzoni mwa mwezi jana huko mjini Dodoma alipokuwa akihudhuria vikao vya bunge. Hivi karibuni, ndugu zake Bw Lissu wameitaka serikali kuvishirikisha vyombo vya upelelezi vya kimataifa kama vinavyoshirikishwa katika mambo mengine ili kuongeza ufanisi katika upelelezi huo.
Jeshi la polisi nalo limeomba lipewe nafasi wa kufanya upelelezi.Tundu Lissu yuko nchini Kenya kwa takribani wiki nne sasa kwa ajili ya matibabu.
No comments:
Post a Comment