Lissu aliyeshambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi akiwa katika makazi yake Area D mjini Dodoma Septemba 7, amelazwa katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya akiendelea na matibabu.
Akizungumza na Mwananchi leo Jumatatu, baada ya kuulizwa kuhusu hali ya Lissu, Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni amesema:
“Kesho saa 5:00 asubuhi nitakuwa na mkutano na waandishi wa habari, nitazungumzia hali ya Lissuna mambo mengine yanayoendelea.”
Baadaye katika taarifa ya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha chama hicho, Tumaini Makene amesema mkutano huo utafanyika makao makuu ya Chadema Kinondoni jijini Dar es Salaam.
“Kupitia Mwenyekiti, Freeman Mbowe chama kitatoa taarifa kwa Taifa kuhusu maendeleo ya Tundu Lissu, mrejesho wa michango, gharama za matibabu,” amesema Makene.
MCL Digital itarusha mkutano huo moja kwa moja ku
No comments:
Post a Comment